The chat will start when you send the first message.
1Katika Yuda Mungu amejulikana,
Katika Israeli jina lake ni kuu.
2Kibanda chake pia kiko Salemu,
Na maskani yake iko Sayuni.
3Huko ndiko alikoivunja mishale ya uta,[#Zab 46:9; Eze 39:9]
Ngao, na upanga, na zana za vita.
4Wewe U mwenye fahari na adhama,[#Eze 38:12]
Toka milima ya mateka.
5Wametekwa wenye moyo thabiti;[#Isa 46:12; Zab 13:3; Yer 51:39]
Wamelala usingizi;
Wala hawakuiona mikono yao
Watu wote walio hodari.
6Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo,[#Kut 15:1; Nah 2:13; Zek 12:4]
Gari na farasi wameshikwa na usingizi mzito.
7Wewe ndiwe utishaye, naam, Wewe;[#Ayu 41:10; Nah 1:6]
Naye ni nani awezaye kusimama ufanyapo hasira?
8Toka mbinguni ulitangaza hukumu;
Nchi iliogopa, ikakaa kimya.
9Mungu aliposimama ili kuhukumu
Na kuwaokoa wapole wa dunia wote pia.
10Maana hasira ya binadamu itakusifu,[#Kut 9:16]
Masalio ya hasira utajifunga kama mshipi.
11Wekeni nadhiri, mkaziondoe[#Mhu 5:4; Zab 68:29]
Kwa BWANA, Mungu wenu.
Wote wanaomzunguka wamletee hedaya,
Yeye astahiliye kuogopwa.
12Yeye huzikata roho za wakuu;[#Zab 68:35]
Na kuwatisha wafalme wa dunia.