The chat will start when you send the first message.
1Msingi wake upo
Juu ya milima mitakatifu.
2BWANA ayapenda malango ya Sayuni
Kuliko maskani zote za Yakobo.
3Umetajwa kwa mambo matukufu,[#Isa 60:1]
Ee Mji wa Mungu.
4Nitataja Rahabu na Babeli
Miongoni mwao wanaonijua.
Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi;
Huyu alizaliwa humo.
5Naam, mintarafu Sayuni itasemwa,[#Eze 48:35; Mt 16:18]
Huyu na huyu alizaliwa humo.
Na Yeye Aliye juu
Ataufanya imara.
6BWANA atahesabu, awaandikapo mataifa,[#Zab 22:30; Isa 4:3; Yer 3:19; Eze 13:9]
Huyu alizaliwa humo.
7Waimbao na wachezao na waseme,
Visima vyangu vyote vimo mwako.