The chat will start when you send the first message.
1Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu,
Kizazi baada ya kizazi.
2Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia,[#Ayu 38:4-6; Mit 8:25]
Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
3Wamrudisha mtu mavumbini,[#Mwa 3:19; Mhu 12:7]
usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
4Maana miaka elfu machoni pako[#Ebr 13:8; 2 Pet 3:8]
Ni kama siku ya jana ikiisha kupita,
Na kama kesha la usiku.
5Wawagharikisha, huwa kama usingizi,[#Isa 40:6]
Asubuhi huwa kama majani yameayo.
6Asubuhi yachipuka na kumea,[#Ayu 14:2; Zab 92:7]
Jioni yakatika na kukauka.
7Maana tumetoweshwa kwa hasira yako,
Na kwa ghadhabu yako tumefadhaishwa.
8Umeyaweka maovu yetu mbele zako,[#Zab 50:21; Yer 16:17; Zab 19:12; Mit 5:21; Mhu 12:14; Rum 2:16; 1 Kor 4:5; Ebr 4:12,13]
Siri zetu katika mwanga wa uso wako.
9Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako,
Tumetowesha miaka yetu kama kite.
10Siku za miaka yetu ni miaka sabini,
Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;
Na kiburi chake ni taabu na ubatili,
Maana chapita upesi tukatokomea mara.
11Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako?
Na ghadhabu yako kama ipasavyo kicho chako?
12Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu,[#Zab 39:4]
Tujipatie moyo wa hekima.
13Ee BWANA urudi, hata lini?[#Kum 32:36]
Uwahurumie watumishi wako.
14Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,
Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
15Utufurahishe kwa kadiri ya siku ulizotutesa,
Kama miaka ile tuliyoona mabaya.
16Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako,[#Zab 44:1; Hab 3:2]
Na adhama yako kwa watoto wao.
17Na uzuri wa BWANA, Mungu wetu, uwe juu yetu,[#Isa 26:12; 2 The 2:16,17]
Na kazi ya mikono yetu utufanyie thabiti,
Naam, kazi ya mikono yetu uithibitishe.