The chat will start when you send the first message.
1Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu,[#Zab 4:6; 6:6; Isa 26:9]
Nalimtafuta, nisimpate.
2Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini,
Katika njia zake na viwanjani,
Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu.
Nikamtafuta, nisimpate.
3Walinzi wazungukao mjini waliniona;[#Wim 5:7; Isa 21:6-8,11,12]
Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?
4Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea,[#Mit 8:17; 4:13; Rum 8:35,39]
Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu;
Nikamshika, nisimwache tena,
Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu,
Chumbani mwake aliyenizaa.
5Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,[#Wim 2:7]
Kwa paa na kwa ayala wa porini,
Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,
Hata yatakapoona vema yenyewe.
6Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani,[#Wim 8:5; Yer 2:2]
Mfano wake ni nguzo za moshi;
Afukizwa manemane na ubani,
Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?
7Tazama, ni machela yake Sulemani;
Mashujaa sitini waizunguka,
Wa mashujaa wa Israeli.
8Wote wameshika upanga,
Wamehitimu kupigana;
Kila mtu anao upanga wake pajani
Kwa hofu ya kamsa za usiku.
9Mfalme Sulemani alijifanyizia machela
Ya miti ya Lebanoni;
10Nguzo zake alizifanyiza za fedha,[#Mt 22:37; Yn 13:1,34; Rum 5:8; Efe 3:19; 1 Pet 1:7,8]
Na mgongo wake wa dhahabu,
Kiti chake kimepambwa urujuani,
Gari lake limenakishiwa njumu,
Hiba ya binti za Yerusalemu.
11Tokeni, enyi binti za Sayuni,[#Ufu 11:15; Zab 110:3; Isa 62:5]
Mtazameni Mfalme Sulemani,
Amevaa taji alivyovikwa na mamaye,
Siku ya maposo yake,
Siku ya furaha ya moyo wake.