The chat will start when you send the first message.
1Laiti ungekuwa kama ndugu yangu,
Aliyeyanyonya matiti ya mamangu!
Kama ningekukuta huko nje,
Ningekubusu, asinidharau mtu.
2Ningekuongoza nyumbani mwa mamangu,[#Mit 9:2]
Naye angenifundisha;
Ningekunywesha divai iliyokolea,
Divai mpya ya mkomamanga wangu.
3Mkono wake wa kushoto ungekuwa chini ya kichwa changu,[#Wim 2:6; Isa 62:4,5; 2 Kor 12:9]
Nao wa kuume ungenikumbatia.
4Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,
Kwani kuyachochea mapenzi, au kuyaamsha,
Hata yatakapoona vema?
5Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani,[#Yn 17:14]
Akimtegemea mpendwa wake?
Nalikuamsha chini ya huo mpera;
Huko mama yako alikuonea utungu,
Aliona utungu aliyekuzaa.
6Nitie kama muhuri moyoni mwako,[#Isa 49:16; Yer 22:24; Hag 2:23; Flp 3:8]
Kama muhuri juu ya mkono wako;
Kwa maana upendo una nguvu kama mauti,
Na wivu ni mkali kama ahera.
Mwako wake ni mwako wa moto,
Na miali yake ni miali ya Yahu.
7Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,[#Mit 6:35]
Wala mito haiwezi kuuzamisha;
Kama mtu angetoa badala ya upendo
Mali yote ya nyumbani mwake,
Angedharauliwa kabisa.
8Kwetu sisi tuna umbu mdogo,[#Zab 22:27]
Wala hana maziwa;
Tumfanyieje umbu letu,
Siku atakapoposwa?
9Kama akiwa tu ukuta,[#Ufu 3:20]
Tumjengee buruji za fedha;
Na kama akiwa ni mlango,
Tumhifadhi kwa mbao za mierezi.
10Mimi nalikuwa ukuta,[#Kol 2:7; Eze 16:7]
Na maziwa yangu kama minara;
Ndipo nikawa machoni pake
Kama mtu aliyeipata amani.
11Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-hamomi[#Mt 21:33]
Akawakodisha walinzi hilo shamba lake la mizabibu;
Kila mtu atoe vipande elfu vya fedha kwa matunda yake.
12Shamba langu la mizabibu, lililo langu mimi, li mbele yangu.
Basi, Sulemani, wewe uwe na elfu zako,
Na hao wayalindao matunda yake wapewe mia mbili.
13Wewe ukaaye bustanini,[#Wim 2:14]
Hao rafiki huisikiliza sauti yako;
Unisikizishe mimi.
14Ukimbie, mpendwa wangu,[#Wim 2:17]
Nawe uwe kama paa, au ayala,
Juu ya milima ya manukato.