1 Wakorintho 12

1 Wakorintho 12

1KWA khabari za karama za roho, ndugu, sitaki mkose kufahamu.

2Mwajua ya kuwa mlipokuwa Mataifa mlichukuliwa kwa sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa.

3Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hapana mtu asemae katika Roho ya Mungu, anenae, Yesu ni anathema; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.

4Pana tofauti za karama; bali Roho yule yule.

5Pana tofauti za khuduma, na Bwana vule yule;

6pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu yule yule azitendae kazi zote katika wote.

7Lakini killa mmoja hupewa ufunuo wa Roho illi kufaidia.

8Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, ipendavyo Roho yule yule;

9mwingine imani katika Roho yule yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;

10na mwingine kutenda kazi za miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;

11lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yule yule, akimgawia killa mmoja peke yake kama apendavyo yeye.

12Maana kama vile mwili ni mmoja, nao nna viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule mmoja, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.

13Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa tukaingia katika mwili mmoja, ikiwa tu Wayahudi, au ikiwa tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

14Kwa maana mwili hauwi kiungo kimoja, bali vingi.

15Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! si wa mwili kwa sababu hiyo?

16Na sikio likisema, Mimi si jicho, mimi si wa mwili; je! si wa mwili kwa sababu hiyo?

17Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? kama wote ni sikio ku wapi kuona?

18Bali Mungu amevitia viungo killa kimoja katika mwili kama alivyotaka.

19Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?

20Lakini sasa viungo ni vingi, na mwili ni mmoja.

21Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina baja na ninyi.

22Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi.

23Na vile vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana.

24Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; hali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima kile kiungo kilichopungukiwa;

25illi kusiwe fitina katika mwili, hali viungo vitunzane.

26Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia navyo, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja.

27Na ninyi m mwili wa Kristo, na viungo vya mwili huo, mmoja hiki na mmoja hiki.

28Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kiisha miujiza, kiisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na kutawala, na aina za lugha.

29Je! wote ni mitume? wote ni manabii? wote ni waalimu? wote wanatenda miujiza?

30wote wana karama za kuponya wagonjwa? wote wanena lugha? wote wafasiri? Takeni sana karama zilizo njema zaidi.

31Na tena nawaonyesha njia iliyo bora sana.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania