1 Wakorintho 16

1 Wakorintho 16

1KWA khabari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisaya Galatia, na ninyi fanyeni vivyo hivyo.

2Siku ya kwanza ya juma killa mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; changizo zisifanyike hapo nitakapokuja:

3nami nitakapofika nitawatuma wale mtakaowachagua kwa nyaraka, wachukue ihsani yenu hatta Yerusalemi.

4Na kama ikifaa niende na mimi, watasafiri pamoja nami.

5Lakini nitakuja kwenu, nikipita kati ya Makedonia; maana napita kati ya Makedonia.

6Labda nitakaa kwenu; naam, labda nitashinda kwenu wakati wa baridi, mpate kunisafirisha wakati uwao wote nitakapokwenda.

7Maana sitaki kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraja kukaa kwenu mda wa kitambo, Bwana akinijalia.

8Lakini nitakaa katika Efeso mpaka Pentekote;

9kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wengi wako wanipingao.

10Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo khofu; maana anaifanya kazi ya Bwana kama mimi nami:

11bassi mtu aliye yote asimdharau, lakini msafirisheni kwa amani, illi aje kwangu; maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu.

12Lakini kwa khabari za Apollo, ndugu yetu, nalimsihi sana aende kwenu pamoja nao ndugu, nae hakupenda kabisa kwenda sasa; lakini atakwenda sitakupopata nafasi.

13Kesheni, simameni imara katika Imani, mwe waume, mwe hodari.

14Mambo yenu yote yatendeke katika upendo.

15Tena nawasihi, ndugu, (mnaijua nyumba ya Stefano kwamba ni malimbuko ya Akaia, nao wamejitia katika kazi ya kuwakhudumu watakatifu),

16bassi watiini watu kama hawa, na killa mtu afanyae kazi pamoja nao, na kujitaabisha.

17Nami nafurahi, kwa sababu ya kuwako kwao Stefano na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikarimia kwa wingi nilivopungukiwa kwenu.

18Maana wamenihurudisha roho yangu, na roho zenu pia; bassi wajueni sana watu kama hao.

19Makanisa ya Asia wawasalimu. Akula na Priskilla wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililo ndani ya nyumba yao.

20Ndugu wote wawasalimu. Kasalimianeni kwa busu takatifu.

21Hii ni salamu yangu mimi Paolo kwa nikono wangu mwenyewe.

22Mtu aliye yote asiyempenda Bwana Yesu Kristo, na awe anathema. Maranatha.

23Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.

24Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu. Amin.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania