The chat will start when you send the first message.
1YAKINI khabari imeenea ya kama kwenu kuna zina, na zina hiyo ya namna isiyonenwa hatta katika mataifa, kwamba mtu awe na mke wa baba yake.
2Nanyi minejivuna wala hamkusikitika illi aondolewe kati yenu yeye aliyetenda jambo hilo.
3Kwa maana mimi kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo.
4Katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na nweza wa Bwana wetu Yesu Kristo,
5kumtolea Shetani mtu huyo, mwili uadhibiwe, illi roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.
6Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulitia chachu donge zima?
7Bassi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, illi mwe donge jipya, kama vule mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka yetu amekwisha kutolewa sadaka kwa ajili yetu, yaani Kristo;
8bassi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochacha, ndio weupe wa moyo na kweli.
9Naliwaandikieni katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi.
10Sisemi msichangamane kabisa kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani an wanyangʼanyi, an wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.
11Lakini sasa nimewaandikieni kwamba msichangamane na mtu aitwae ndugu, akiwa mzinzi au mwenye kutamani an mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnangʼanyi; mtu wa namna hii msikubali hatta kula nae.
12Maana yanikhusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu walio ndani?
13Bali hao walio nje Mungu atawahukumu. Mwondoeni mtu yule mbaya, asikae kwenu.