1 Wakorintho 7

1 Wakorintho 7

1BASSI kwa mambo yale mliyoniandikia, ni kheri mwanamume asiguse mwanamke.

2Lakini kwa sababu ya mambo ya zina killa mtu na awe na mke wake mwenyewe, na killa mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

3Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.

4Mke hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mume wake; na vivyo hivyo mume hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mke wake.

5Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, illi mpate faragha kwa kufunga na kuomba, mkajiane tena, Shetani asije akawajarihu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.

6Lakini nasema haya, nikitoa idhini yangu; sitoi amri.

7Maana nipendalo ni watu wote wawe kama mimi nilivyo; illakini killa mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.

8Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni kheri wakae kama mimi nilivyo.

9Lakini kama hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka moto.

10Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza, wala si mimi, illa Bwana, mke asiachane na mumewe;

11lakini, ikiwa ameachana nae, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.

12Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana; ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke buyo anakubali kukaa nae, asimwache.

13Na mwanamke, ambae ana mume asiyeamini, mume huyo na anakubali kukaa nae, asimwache.

14Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa kwa mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa kwa mumewe; kama isingekuwa bivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.

15Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo ndugu mume au ndugu mke hafungiki.

16Lakini Mungu ametuita katika amani. Kwa maana wajuaje, ee mwanamke, kama ntamwokoa mume wako? au wajuaje ee mwanamume, kama utamwokoa mke wako?

17Lakini Mungu alivyomgawia killa mtu—kama Mungu alivyomwita killa mtu, na aenende vivyo hivyo. Na ndivyo ninavyoagiza katika Makanisa yote.

18Mtu fullani ameitwa nae amekwisha kutahiriwa? asijifanye kana kwamba hakutabiriwa. Mtu fullani amekwitwa nae hajatahiriwa bado? bassi asitahiriwe.

19Kutabiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu; bali kuzihifadhi amri za Mungu.

20Killa mtu na akae katika hali ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa.

21Je! ulikwitwa u mtumwa? usione ni vibaya; lakini kama ukiweza kuwa na uburu, afadhali kuutumia.

22Kwa maana yeye aliyekwitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye nae aliyekwitwa hali ya uhuru, ni mtuniwa wa Kristo.

23Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wana Adamu.

24Killa mtu, ndugu zangu, na akae katika hali hiyo hiyo aliyoitwa.

25Kwa khabari za mabikira sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kuwa mwaminifu kwa rehema za Bwana.

26Bassi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shidda hii tuliyo nayo, kwamba ni vyema mtu akae kama alivyo.

27Umefungwa kwa mke? usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? usitafute mke.

28Lakini, kama ukioa, huna khatiya, na bikira akiolewa, hana khatiya; lakini watu hao watakuwa na mateso katika mwili; lakini nataka kuwazuilia haya.

29Lakini, nasema hivi, ndugu, muda ubakio si mwingi; bassi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;

30na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi: na wale wanunuao, kama hawana kitu.

31Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.

32Lakini nataka inwe hamna masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;

33bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.

34Tena iko tofauti hii kati ya mke na hikira. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu katika mwili na katika roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia, jinsi atakavyompendeza mumewe.

35Nasema haya niwafaidie; si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, na mpate kumkhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.

36Lakini mtu awae yote akiona ya kuwa hamtendei bikira wake vipendezavyo, na ikiwa amepita uzuri wa ujana wake, na kama pana haja, bassi, afanye apendavyo, hafanyi dhambi; na waoane.

37Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuitawala nia yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda bikira wake, atenda vyema.

38Bassi, amwozae bikira wake afanya vyema; na yeye asiyemwoza afanya vyema zaidi.

39Mwanamke hufungwa maadam mumewe yu hayi, lakini iki va mumewe amefariki, yu huru; aweza kuolewa na mtu ye yote amtakae; katika Bwana tu.

40Lakini yu kheri zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi; nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho ya Bwana.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania