1 Yohana 1

1 Yohana 1

1ILIYOKUWA tangu mwanzo, tuliyoisikia, tuliyoiona kwa macho yetu, tuliyoitazama, na mikono yetu ikaipapasa, kwa khabari ya Neno la uzima,

2(na uzima buo ulidhihirika, nasi tumeona, na twashuhudu, na twawakhubirini ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);

3tuliyoiona na kuisikia, twawakhubiri ninyi; ninyi nanyi mpate kushirikiana na sisi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.

4Na haya twawaandikieni, illi furaha yenu itimizwe.

5Na hii ndiyo khabari tuliyoisikia kwake, na kuikhubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza yo yote hamna ndani yake.

6Tukisema twashirikiana nae, tena tukienenda gizani, twasema uwongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;

7bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwana wake, yatusafisha dhambi zote.

8Tukisema hatuna dhambi, twajidanganya, wala kweli haimo mwetu.

9Tukiziungama dhambi zetu, yu amini na wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha udhalimu wote.

10Tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya mwongo wala neno lake halimo mwetu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania