The chat will start when you send the first message.
1WATOTO wangu wadogo, nawaandikia haya illi msitende dhambi. Na ijapo mtu akatenda dhambi tuna Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
2nae ni kipatanisho kwa dhambi zetu: wala si kwa dhambi zetu tu, bali kwa dhambi za ulimwengu wote.
3Na hivi twajua ya kuwa tumemjua, ikiwa tunashika amri zake.
4Yeye asemae, Nimemjua, nae hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake.
5Lakiui yeye alishikae neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Ilivi twajua ya kuwa tumo ndani yake.
6Yeye asemae ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vilevile kama yeye alivyoenenda.
7Ndugu, siwaandikii amri mpya, illa amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo.
8Na ile amri ya zamani ndiyo ile mliyosikia tangu mwanzo. Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kungʼaa.
9Yeye asemae kwamba yumo katika nuru, nae amchukia ndugu yake, yumo gizani hatta sasa.
10Yeye ampendae ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.
11Bali yeye amchukiae ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.
12Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake.
13Nawaandikia, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nawaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba.
14Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu m hodari, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu.
15Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16Maana killa kilichomo duniani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, hazitokani na Baba, bali zatokana ua dunia.
17Na dunia inapita, na tamaa yake, bali yeye afanyae mapenzi ya Mungu adumu hatta milele.
18Watoto, ni wakati wa mwisho: na kama vile mlivyosikia kwamba adui wa Kristo yuaja, hatta sasa adui wengi wa Kristo wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.
19Walitoka kwetu, bali hawukuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka illi wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.
20Na ninyi mmepakwa mafuta nae aliye Mtakatifu na mnajua yote.
21Sikuwaandikia ninyi, kwa sababu hamwijui kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uwongo wo wote utokao katika kweli.
22Naui aliye mwongo illa yeye akanae ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye adui wa Kristo, amkanae Baba na Mwana.
23Killa anikanae Mwana, amkana Baba pia.
24Bassi, na yakae ndani yenu maneno yale mliyoyasikia tangu mwanzo. Neno lile mlilolisikia tangu mwanzo likikaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.
25Na hii ndiyo ahadi alivyowaahidia ninyi, uzima wa milele.
26Nimewaandikia haya katika khabari za watu wale wanaotaka kuwapoteza.
27Na ninyi, mafuta, yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, nanyi hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama yale mafuta yanavyokufundisheni khabari za mambo yote, tena ni kweli wala si uwongo, na kama yalivyokufundisheni, mnakaa ndani yake.
28Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, illi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibishwe mbele zake katika kuja kwake.
29Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa killa atendae haki amezaliwa nae.