The chat will start when you send the first message.
1KILLA mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na killa mtu ampendae mwenye kuzaa ampenda na yeye mwenye kuzaliwa nae.
2Hivi twajua kwamba twawapencla watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.
3Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kuzisinka amri zake: na amri zake si nzito.
4Kwa maana killa kitu kilihozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, imani yetu.
5Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa yeye aaminiye ya kwamba Yesu yu Mwana wa Mungu?
6Huyu ndiye ajae kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Na Roho ndiyo ishuhuduyo, kwa sababu Roho ndiyo iliyo kweli.
7Kwa maana watatu ni mashahidi mbinguni, Baba, Neno, na Robo Mtakatifu, ua watatu hawa ni umoja.
8Maana watatu ndio washuhuduo duniani, roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupataua kwa khabari moja.
9Tukiupokea ushuliuda wa wana Adamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, amemshuhudia Mwana wake.
10Amwaminiye Mwana wa Mungu anao ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu amemsbuhudia Mwana wake.
11Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwana wake.
12Aliye nae Mwana, ana uzima; asiye nae Mwana wa Mungu hana uzima.
13Nimewaandikia mambo haya, illi mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.
14Na huu ndio njasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu kama vile apendavyo, atusikia:
15Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombapo cho chote, twajua kwamba tunazo zile dua tulizomwomba.
16Mtu akimwona ndugu yake anakosa kosa lisilo la mauti, ataomba, nae atampa uzima kwa ajili ya hawo wakosao kosa lisilo la mauti. Liko kosa lililo la mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hilo.
17Killa lisilo la haki ni kosa, na kosa liko lisilo la mauti.
18Twajua ya kuwa killa mtu aliyezaliwa na Mungu hakosi: bali yeye aliyezaliwa na Mungu ajilinda, na yule mwovu hamgusi.
19Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.
20Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.
21Watoto wangu wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.