1 Petro 2

1 Petro 2

1BASSI, mkiwekea mbali uovu wote na hila yote na unafiki na husuda na niasingizio yote,

2kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, illi kwa hayo mpate kunkulia wokofu;

3ikiwa mmeonja kwamba Bwana ni mwenye fadhili.

4Mkimwendea yeye, jiwe lililo hayi, lililokataliwa na wana Adamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye thamani,

5ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hayi, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani utakatifu, mtoe dhabibu za roho, zipatazo kibali kwa Mungu, kwa Yesu Kristo.

6Kwa kuwa ndiyo yaliyomo katika maandiko,

Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye thamani,

Na killa amwaminiye hatatabayarika.

7Bassi, thamani hii ni kwenu ninyi mnaoamini, bali kwao wasioamini,

Jiwe walilolikataa waashi,

Limekuwa jiwe kuu la pembeni;

8tena,

Jiwe lakujikwaza mguu, na mwamba wa kujiangusha; maana hujikwaza kwa neno lile, wakiliasi, nao waliwekwa wapate hayo.

9Bali ninyi m mzao mteule, ukubani wa kifaume, taifa takatifu, watu wa milki, mpate kutangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

10ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

11Mapenzi, nakusihini kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho;

12mwe na maongezi mazuri kati ya Mataifa, illi, iwapo huwasingizia kuwa mnatenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa nae.

13Tumikieni killa kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa mfalme, kama mwenye cheo kikuliwa;

14ikiwa wakubwa, kama wanaotumwa nae kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema;

15kwa sababu ndio mapenzi ya Mungu, kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;

16kama huru, na wasiontumia uhuru kwa kusetiri ubaya, bali kaina watumwa wa Mungu.

17Heshimuni walu wote. Upendeni udugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.

18Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa khofu nyingi; sio wao walio wema na wenye upole fu, bali nao walio wakali.

19Maana huu ndio wema khassa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, ateswapo isivyo baki.

20Kwa maana ni sifa gani kuvumilia, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kuvumilia, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema khassa mbele za Mungu.

21Kwa sababu ndio mlioitiwa: maana Kristo nae aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachieni mfano, mfuate nyayo zake;

22yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake;

23yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki;

24yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, illi, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe bayi kwa mambo ya haki; kwa kuchubuka kwake mliponywa.

25Kwa maana mlikuwa kama kondoo wanaopotea; lakini sasa mmemrudia Mchunga na Askofu wa roho zenu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania