The chat will start when you send the first message.
1BASSI kwa biyo, tulipokuwa hatukuweza kuvumilia zaidi, tuliona vema kuachwa Athene peke yetu;
2tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu, mfanya kazi pamoja naswi katika Injili ya Kristo, kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa ajili ya imani yenu,
3mtu asifadhaishwe na mateso haya: maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa haya.
4Kwa maana tulipokuwa kwenu tulitangulia kuwaambieni kwamba tutapata kuteswa, kama ilivyotukia, nanyi mwajua.
5Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalimtuma mtu illi niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, wala taabu yetu isiwe haina faida.
6Lakini Timotheo alipotujia siku hizi kutoka kwenu, akatuletea khabari njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote: mkitamani kutuona sisi vile vile kama sisi ninyi;
7kwa sababu hiyo tulifarijiwa, ndugu, kwa khabari zenu, katika shidda na mateso yetu yote, kwa imani yenu.
8Kwa kuwa sasa twaishi, ikiwa ninyi mnasimama imara katika Bwana.
9Maana shukrani gani tuwezayo kumlipa Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha ile yote tunayoifurahia, kwa sababu yenu mbele za Mungu wetu;
10usiku na mchana tukiomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu na kuyatengeneza mapungufu ya imani yenu.
11Bassi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu Kristo atuongoze njia yetu tufike kwenu;
12Bwana na awaongozeni na kuwazidisheni katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile na sisi kwenu;
13apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.