1 Wathessaloniki 4

1 Wathessaloniki 4

1ILIYOBAKI, ndugu, tunakusihini na kukuonyeni kuenenda katika Bwana Yesu, kama mlivyopokea kwetu, jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama na muavyoenenda, mpate kuzidizidi sana.

2Maana mnajua maagizo gani tuliyowapeni kwa Bwana Yesu.

3Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na nasharati;

4killa mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima,

5si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu;

6mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizae kisasi cha haya yote, kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudu sana.

7Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.

8Bassi yeye anaekataa, hakatai mwana Adamu bali Mungu, anaewapeni Roho yake Mtakatifu.

9Kwa khabari ya upendano, hamna haja niwaandikie: maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.

10Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia wote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana;

11tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe kama tulivyowaagiza;

12illi mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na baja ya cho chote.

13Lakini, ndugu, hatutaki msijue khabari zao waliolala, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.

14Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu Mungu atawaleta pamoja nae.

15Maana twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hayi, tutakaosalia hatta wakati wa kuja kwake Bwana, hatutawatangulia wao waliokwisha kulala.

16Kwasababu Bwana mwenyewe atasbuka kutoka mbinguni na sauti kuu na sauti ya malaika mkuu, na panda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo, watafufuliwa kwanza;

17baada va haya sisi tulio hayi, tuliosalia, tutachukuliwa pamoja nao katika mawingu, illi tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

18Bassi, farijianeni kwa maneno haya.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania