1 Timotheo 2

1 Timotheo 2

1BASSI, kabla ya mambo yote, dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;

2kwa ajili ya wafalme, na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya ntulivu na amani, katika utawa wote, na ustahifu.

3Maana hili ni zuri, lenye kibali mbele za Mwokozi wetu Mungu

4atakae watu wote waokolewe wakapate kujua sana yaliyo kweli.

5Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wana Adamu ni mmoja, mwana Adamu, Kristo Yesu,

6aliyejitoa nafsi yake kuwa ukombozi kwa ajili ya wote utakaoshuhudiwa kwa majira yake;

7kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mkhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo, sisemi uwongo), mwalimu wa mataifa katika imani na kweli.

8Bassi nataka wanaume waombe killa mahali, wakimua mikono mitakatifu, pasipo hasira na majadiliano.

9Na vivyo hivyo wanawake wajipambe kwa mavazi ya kujisetiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi, si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

10bali kama iwapasavyo wanawake wanaokiri utawa, kwa matendo mema.

11Mwanamke na ajifunze kalika utulivu, akitii kwa killa namna.

12Simpi mwanamke rukhusa kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali kuwa katika utulivu.

13Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadae.

14Na Adamu hakudanganywa, bali mwanamke akidanganywa aliingia hali ya kukosa.

15Lakini ataokolewa, kwa ule uzazi, kama wakidumu katika imani na npendo na utakatifu pamoja na moyo wa kiasi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania