1 Timotheo 6

1 Timotheo 6

1WO wote waiio chini ya mafungo, hali ya utumwa, wawahesabu bwana zao kuwa wamestahili heshima yote, jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.

2Na wale walio na mabwana waaminio, wasiwadharau kwa kuwa ni ndugu; hali afadhali wawatumikie, kwa sababu hao waishirikio faida ya kazi zao wamekuwa wenye imani na kupendwa. Uwafundishe mambo haya, na kuonya.

3Mtu akifundisba mafundisho mengine, nae hayakubali maneno yenye afya va Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundislio yapatanayo na ntawa,

4amejivuna, nae hakufahamu neno lo lote, bali hali yake hali va ugonjwa, kwa khabari ya maswali na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya,

5na majadiliano ya watu walioharibiwa akili zao, walioikosa kweli, wakidhani ya kuwa utawa ni njia ya kupata faida; ujitenge na watu kama hao,

6Lakini utawa pamoja na kuridhia ni faida nyingi.

7Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena ni dhahiri va kuwa hatuwezi kutoka na kitu

8bali tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.

9Watakao kuwa na mali waanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa zisizo maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wana Adamu katika upotevu na uharibifu.

10Maana shina moja la mabaya yote ni kupenda fedha, ambayo wengine wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani na kujichoma kwa maumivu mengi.

11Bali wewe, mtu wa Mungu, yakimbie hayo, ukafuate haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu, upole.

12Fanya vita vile vizuri vya imani, shika uzima wa milele ulioitiwa, ukayaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.

13Nakuagiza mbele za Mungu avipae vitu vyote uzima, na mbele za Kristo Yesu aliyeungama maungamo yale mazuri mbele ya Pontio Pilato,

14ilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hatta kudhihiri kwake Bwana wetu Yesu Kristo,

15ambako katika nyakati zake mwenyewe ataonyesha yeye mwenye uweza wote, Mfalme wa Wafalme, Bwana wa Mabwana,

16ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin.

17Uwaagize walio matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, wala wasitumainie utajiri usio yakini, bali Mungu aliye hayi atupae vitu vyote kwa wingi, tuvitumie kwa furaha;

18watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo,

19wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao illi wapate uzima wa milele.

20Timotheo, ilinde amana, ukijiepisha na maneno yasiyo ya dini, yasiyo maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa nwongo;

21wengine wakiikiri hiyo wameikosa Imani.

Neema na iwe pamoja nawe.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania