The chat will start when you send the first message.
1SINA buddi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia njozi na mafunuo ya Bwana.
2Namjua mtu mmoja katika Kristo, impita sasa miaka arobatashara, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui, Mungu ajua). Mtu huyu alichukuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
3Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui: Mungu ajua):
4ya kuwa alichukuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwana Adamu ayanene.
5Kwa khabari za mtu huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika khabari ya udhaifu wangu.
6Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini nitajizuia, mtu asinihesabie zaidi ya haya ayaonayo kwangu au kuyasikiakwa kinywa changu.
7Na kwa sababu ya wingi wa mafunuo hayo, kwa sababu hiyo, nisipate kujivuna kupita kiasi, nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani illi anipige, nisije mkajivuna kupita kiasi.
8Kwa ajili ya kitu hiki nalimsihi Bwaua marra tatu kinitoke.
9Akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Bassi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, illi uweza wa Kristo ukae juu yangu.
10Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na maumivu, na dhiiki, na adha, na shidda, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo ua nguvu.
11Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu, nijapokuwa si kitu.
12Maana ishara za mtume zilitendwa kati yenu katika uvumilivu wote, kwa ishara na maajabu na nguvu.
13Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, illa kwa kuwa mimi sikuwalemea. Mnisamehe udhalimu huo.
14Tazama hii ni marra ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawidemea. Maana sitafuti vitu vyenu, bali ninyi: maana haiwapasi watoto kuwawekea akiba wazazi, bali wazazi watoto.
15Na kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu: ingawa nizidipo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?
16Lakini na iwe hivyo, mimi sikuwalemea; bali kwa kuwa mwerevu naliwapata kwa hila.
17Je! mtu aliye yote niliyemtuma kwenu, kwa mtu huyo naliwatoza kitu?
18Nalimwonya Tito, nikamtuma yule ndugu pamoja nae. Je! Tito aliwatoza kitu? Hatukuenenda kwa Roho yeye yule na katika nyayo zile zile?
19Mwadhani ya kuwa tunajindhuru kwenu tena? Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na haya yote, wapenzi, kwa ajili ya kuwajenga.
20Maana naogopa, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekane kwenu si kama vile mtakavyo: nisije nikakuta labuda fitina, na wivu, na hasira, na ugomvi, na masingizio, na manongʼonezo, na majivuno, na ghasia;
21nami nitakapokuja tena, Mungu wangu akanidhili kwenu, nikawasikitikia wengi waliokosa zamani, wala hawakutubia nchafu, na uzinzi, na uasharati walioufanya.