The chat will start when you send the first message.
1KWA khabari za kuwakhudumia watakatifu sina haja ya kuwaandikia.
2Maana najua utajiri wenu, niliojisifia kwa Wamakedoni, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo watu wengi.
3Lakini naliwatuma ndugu, illi kujisifu kwangu kwa ajili yenu kusibatilike katika jambo hili; mpate kuwa tayari, kama nilivyosema:
4kusudi, wakija Wamakedoni pamoja nami, na kuwakuta hamjawa tayari, tusije tukatahayarika sisi, tusiseme ninyi, katika hali hii va kutumaini.
5Bassi naliona ya kuwa ni lazima niwaonye ndugu hawa watangulie kufika kwenu, na kutengeneza mapema karama yenu mliyoahidi tangu zamani, illi iwe tayari, na hivi iwe kama kipawa, wala si kama kitu kitolewacho kwa choyo.
6Lakini nasema neno liili, Apandae haha atavuna haha; apandae kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
7Killa mtu na atende alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoae kwa moyo wa ukunjufu.
8Na Mungu aweza kuwajaza killa neema kwa wingi, illl ninyi, mkiwa na riziki za killa namna siku zote, mpate kuzidi sana katika killa tendo jema;
9kama ilivyoandikwa,
Ametapanya, amewapa maskini,
Haki yake yakaa milele.
10Na yeye amruzukuye mbegu mwenye kupanda, atoae mkate uwe chakula, atawapeni mbegu za kupanda na kuzizidisha, atayaongeza mazao ya haki yenu;
11mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.
12Maana utumishi wa khuduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu;
13kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huu, mnamtukuza Mungu kwa ajili ya ntii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.
14Nao wenyewe, wakiwaombea ninyi, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sanu ndani yenu.
15Mungu ashukuriwe kwa sababa ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu ipasavyo.