The chat will start when you send the first message.
1MZEE kwa bibi mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na ndugu wote waijuao ile kweli;
2kwa ajili ya ile kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hatta milele.
3Neema, na rehema, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana wetu Yesu Kristo zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.
4Nalifurahi mno kwa kuwa naliwaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.
5Na sasa, Bibi, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.
6Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Illi ndiyo ile amri, kama ulivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.
7Kwa maana wadanganyifu wengi wameingia katika dunia, wasio-ungama ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na adui wa Kristo.
8Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu.
9Killa aendeleae mbele, asidumu katika ma-fundisho ya Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho ya Kristo, mtu huyu ana Baba na Mwana pia.
10Mtu akija kwenu, nae haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.
11Maana ampae salamu azishirika kazi zake mbovu.
12Kwa kuwa nina maneno mengi ya kuwa-andikia, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraja kuja kwenu, na kusema nanyi mdo-mo kwa mdomo, illi furaha yenu itimizwe.
13Wa-toto wa ndugu yako aliye mteule, wakusalimu.