Petro 2

Petro 2

1LAKINI kuliondoka manabii wa uwongo katika watu, kama vile kwenu kutakavyokuwa waalimu wa uwongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hatta Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu nsiokawia.

2Na wengi watafuata jeuri zao; kwa hawo njia ya kweli itanenwa unajisi.

3Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa: hukumu yao tangu zamani haikawii, wala upotevu wao hausinzii.

4Kwa maana kama vile Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika mafungo ya giza, walindwe hatta ije hukumu;

5wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa wasiomeha Mungu,

6akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipiudua ua kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;

7akamwokoa Lut, aliyehuzunishwa na mwenendo wa uasharati wa hawo wakhalifu;

8maaua mtu huyu mwenye haki akikaa kwao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sharia:

9Bwana ajua kuwaokoa wamchao na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hatta siku ya hukumu;

10na khassa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu, na kudharau mamlaka. Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu;

11ijapokuwa malaika, walio wakuu zaidi kwa uwezo na nguvu, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele ya Bwana.

12Lakini hawo kama nyama wasio na akili, kwa asili yao watu wa kukamatwa kama nyama na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;

13wakipatwa na madhara, ujira wa udhalimu wao, wakidhani kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; ni mawaa na aibu, wakifuata anasa katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;

14wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kukhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo ilivozoezwa kutamani, wana wa laana;

15walioiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaam, mwana wa Bosor, aliyependa ujira wa ndhalimu:

16lakini alikaripiwa kwa ukhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule.

17Hawa ni visiwa visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa:

18wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu:

19wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu. Maana mtu akishindwa na mtu, huwa mtumwa wa mtu yule.

20Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua sana Bwana, Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.

21Maana ingekuwa kheri kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua ile amri takatifu waliyopewa na kuiacha.

22Lakini lile onyo la ile methali ya kweli limewapata: Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa kujifingirisha matopeni.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania