2 Timotheo 3

2 Timotheo 3

1LAKINI ujue neno hili, ya kuwa siku za mwisho zitakuwa nyakati za khatari.

2Maana watu walakuwa wenye kujipenda nafsi zao, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kufuru, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao,

3wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,

4makhaini, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko Mungu;

5wenye mfano wa utawa, lakini wakikana nguvu zake; ujiepushe na hao.

6Kwa maana katika hawa wamo wale wajiingizao kalika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi,

7wakijifunza siku zote, wasiweze kabisa kufikia ujuzi wa kweli.

8Vile vile kama Yanne na Yambre walivyopingana na Mnsa, vivyo hivyo na hawa wapingana na kweli, ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.

9Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote kama na wa hao ulivyokuwa.

10Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na upole, na upendo, na uvumilivu,

11tena adha zangu na mateso yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Lustra; killa namna ya adha niliyoistahimili: nae Bwana akaniokoa katika yote.

12Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya ntawa katika Kristo Yesu wataudhiwa.

13Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na wakidanganyika.

14Bali wewe ukae katika yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni nani ambae ulijifunza kwake,

15na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, yawezayo kukuhekimisha hatta upate wokofu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.

16Killa andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibu katika haki;

17illi mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa illi atende killa tendo jema.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania