2 Timotheo 4

2 Timotheo 4

1NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake;

2likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.

3Maana ntakuja wakati watakapoikataa elimu yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti,

4nao watajiepusha na kusikia yaliyo kweli watageukia hadithi za uwongo.

5Bali wewe erevuka katika yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mwinjilisti, timiliza khuduma yako.

6Maana mimi sasa namiminwa, na siku ya kufunguliwa kwangu imekaribia.

7Nimevifanya vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;

8baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.

9Jitahidi kuja kwangu upesi;

10maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu wa sasa, akasafiri kwenda Thessaloniki; Kreske Galatia, Tito Daimatia.

11Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe; maana anifaa kwa kazi ya khuduma.

12Lakini Tukiko nalimpeleka Efeso.

13Joho lile nililomwachia Karpo Troa, ujapo, lete, navyo vitabu, zaidi vile vya ngozi.

14Iskander mfua shaba alinionya mabaya mengi; Bwana atamlipa kwa jinsi ya matendo yake.

15Nawe ujibadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu.

16Katika jawabu yangu ya kwauza hakuna mtu aliyesimama pamoja nami, bali wote waliniacha; wasihesabiwe khatiya kwa jambo bili.

17Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, illi kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, mataifa wrote wakasikie; nikaokolewa katika kanwa la simba.

18Na Bwana ataniokoa na killa neno baya na kunihifadhi hatta uje ufalme wake wa milele.

19Nisalimie Priska, na Akula, na nyumba ya Onesiforo. Erasto alikaa Korintho.

20Trofimo nalimwacha Mileto, hawezi.

21Jitahidi kuja kabla ya wakati wa baridi.

Eubulo akusalimu, na Pudente, na Lino, na Klaudia, na ndugu wote pia.

22Bwana Yesu Kristo awe pamoja na roho yako. Neema na iwe nanyi. Amin.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania