Wakolossai 2

Wakolossai 2

1MAANA nataka muijue juhudi niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili, jinsi ilivyo kuu;

2illi wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo,

3ambae ndani yake zimo hazina zote za hekima na maarifa, zimesetirika.

4Nasema neno hili, mtu asije akawadanganyeni kwa maneno yaliyotungwa illi kuwakosesha.

5Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, illakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.

6Bassi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye,

7mmetia mizizi, na kujengwa katika yeye: mmefanywa imara kwa imani, kaina mlivyofundishwa, mkizidi kutoa shukrani.

8Angalieni intu asiwateke kwa filosofia yake na madanganya matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wana Adamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.

9Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa namna ya kimwili.

10Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi vote na mamlaka.

11Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mkono, kwa kuuvua mwili wa dhambi, wa nyama, kwa tohara ya Kristo;

12mkizikwa pamoja nae katikti ubatizo, katika huo mlifufuliwa pamoja nae, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.

13Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hayi pamoja nae, akiisba kuwasameheni makosa yote;

14akiisba kuifuta ile khati iliyoandikwa na kutushitaki kwa hukumu zake; iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwe kati kati yetu sisi na yeye, akaikaza msalabani;

15akiisha kuziteka enzi na mamlaka, na kuzimithilisha kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.

16Bassi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au viuvwaji au kwa sababu ya siku kuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

17mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

18Mtu asiwanyangʼanye thawabu yenu, akijinyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kwa kuwaabudu malaika, akijishughulisha na asiyoyaona, akijivuna burre, kwa akili ya mwili wake,

19wala hakishiki kiehwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua mkuo utokao kwa Mungu.

20Bassi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkaacha mafundisho ya awali ya ulimwengu, ya nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,

21Msishike, msionje, msiguse;

22(Mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa), mkifuata maagizo na mafundislio ya wana Adamu?

23Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kujinyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali: illakini hayafai kitu wala kuwa dawa ya tamaa za mwili.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania