Wagalatia 3

Wagalatia 3

1ENYI Wagalatia msio akili, ni nani aliyewaloga, msiisadiki kweli, ninyi ambao Kristo aliwekwa mbele ya macho yemi ya kuwa amesulibiwa?

2Nataka kujifunza neno bili moja kwenu. Mlipokea Roho kwa matendo ya sharia, au kwa kusikia kunakotokana na imani?

3Je! m wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa kwa mwili?

4Mmepatikana na mateso makubwa namna hii burre? ikiwa ni burre.

5Bassi, yeye awaruzukiae Roho na kufanya miujiza kati yenu, afanya hayo kwa matendo ya sharia, au kwa kusikia kunakotokana na imani?

6Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa kuwa ana haki.

7Jueni bassi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio walio wana wa Ibrahimu.

8Na andiko, likiona tangu zamani kwamba Mungu atawafanyizia mataifa wema kwa imani, lilimkhubiri Ibrahimu Injili zamani, ya kama, Kwa wewe mataifa yote yatabarikiwa.

9Bassi walio wra imani wabarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwaminifu.

10Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sharia, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu asiodumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sharia, ayafanye.

11Ni dhahiri ya kwamba hapana mtu ahesabiwae kuwa ana haki nibele za Mungu katika sharia; kwa sababu Mwenye haki ataisbi kwa imani.

12Na sharia haikuja kwa imani, bali, Mtu atendae hayo ataishi katika hayo.

13Kristo alitukomboa na laana ya sharia, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu: maaua imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu atuudikwae juu ya mti:

14illi baraka ya Ibrahimu iwafikilie mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupewa ahadi ya Roho kwa njia ya imani.

15Ndugu, nanena kwa jiusi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwana Adamu, illakini likiisha kuthuimtika, hapana mtu alibatilishae, wala kuliongeza neno.

16Ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa uzao, kana kwamba ni watu wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani Kristo.

17Nisemayo ni haya; agano lililofanywa imara kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka aruba mia na thelathini baadae hailitangui, hatta kuibatilisha abadi.

18Kwa maana urithi nkiwa kwa sharia, hauwi tena kwa abadi; lakini Mungu alimkarimia Ibrahimu kwa abadi.

19Torali ni nini bassi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hatta mzao atakapokuja aliyepewa ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe.

20Aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja.

21Bassi, torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha. Kwa kuwa, kama ingalitolewa sharia iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sharia.

22Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi waaminio wapewe ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.

23Lakini kabla ya kuja imani tulikuwa tumewekwa chini ya sharia, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.

24Na hivyo sharia imekuwa mwalimu wa kutuleta kwa Kristo, illi tufanyiziwe wema kwa imani.

25Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini va mwalimu.

26Maana ninyi nyote ni wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.

27Maana ninyi nyote mliobatizwa na kuingizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.

28Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.

29Na kama ninyi ni wa Kristo, bassi, nimekuwa mzao wa Ibrahimu, na wrarithi kwa ahadi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania