Waebrania 1

Waebrania 1

1KWA sehemu nyingi na kwa namna nyingi Mungu zamani alisema na babu zetu katika manabii,

2mwisho wa siku bizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi yote, kwa yeye aliufanya ulimwengu.

3Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;

4amefanyika bora sana kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko wao.

5Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Mwana wangu ndiwe, mimi leo nimekuzaa? na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, na yeye kwangu mwana?

6Hatta amletapo tena mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, anena, Na malaika wote wa Mungu wamsujudu.

7Na katika khabari za malaika anena, Afanyae malaika zake kuwa pepo, na watumislii wake ndimi za moto.

8Lakini katika khabari ya Mwana anena, Kiti chako, Mungu, ni cha milele; na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya kunyoka.

9Umependa haki, umechukia maasi: kwa sababu hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, mafuta ya shangwe kupita wenzako.

10Na, wewe, Bwana, mwanzo umeitia misingi ya inchi, na mbingu ni kazi za mikono yako;

11hizi zitaharibika, na wewe hukaa; hizi zitachakaa kama nguo,

12na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; lakini wewe u yeye yule, na miaka yako haitakoma.

13Je! yuko malaika aliyeambiwa nae maneno haya wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume hatta nitakapoweka adui zako chiui ya nyayo zako?

14Hawo wote si roho zitumikazo, wakitumwa kuwakhudumu wale watakaourithi wokofu?

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania