The chat will start when you send the first message.
1UPENDANO na udumu.
2Msisahau kuwafadhilia wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.
3Wakumbukeni waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; nao wanaodhulumiwa, kwa kuwa nanyi m katika mwili.
4Ndoa iheshimiwe na watu wote, na malalo yawe safi: kwa maana waasharati na wazinzi Mungu atawahukumu.
5Msiwe na tabia ya kupenda fedha: mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.
6Hatta twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiae, sitaogopa: mwana Adamu atanitenda nini?
7Wakumbukeni wale waliokuwa na mamlaka juu yenu, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa maisha zao, iigeni imani yao.
8Yesu Kristo, jana na leo yeye yule na hatta milele.
9Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.
10Tuna madhbahu ambayo wale waikhudumiao khema bawana rukhusa kula vitu vyake.
11Maana nyama wale ambao damu yao ludetwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kituo.
12Kwa ajili hii Yesu nae, illi awatakase watu wake kwa damu yake miwenyewe, alitesyia nje ya mlango.
13Bassi na twende kwake nje ya kituo, tukichukua laumu lake.
14Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.
15Bassi na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo ya watu waliungamao jina lake.
16Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana na watu; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
17Watiini walio na mamlaka juu yenu, na kujinyenyekea kwao; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, illi wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.
18Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote.
19Nami nawasihini zaidi sana kufanya hayo illi nirudishwe kwenu upesi.
20Bassi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka wafu Mchungaji wa kondoo aliye mkuu, kwa damu ya agano la milele, Bwana wetu Yesu,
21awafanye kuwa wrakamilifu katika killa tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, nae akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amin.
22Nawasihini, ndugu, livumilieni neno hili lenye maonyo; maana nimewaandikia kwa maneno machache.
23Jueni ya kuwa ndugu yetu Timotheo amekwisha kufunguliwa; pamoja nae nitawaoneni, kama akija upesi.
24Wasalimuni wote walio na mamlaka juu yenu, na watakatifu wote; walio wa Italia wanakusalimuni.
25Neema na iwe nanyi nyote. Amin.