Waebrania 5

Waebrania 5

1MAANA killa Kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wami Adamu amewekwa kwa ajili ya wana Adamu katika mambo yamkhusuyo Mungu, illi atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;

2awezae kuwachukulia wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika liali ya udhaifu;

3na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi.

4Na hapana mtu ajitwaliae heshima hii, illa yeye aitwae na Mungu kama vile Harimi.

5Vivyo hivyo Kristo nae hakujitukuza nafsi yake kufanywa Kuhani mkuu, lakini yeye aliyenena nae:

Mwana wangu ni wewe,

Mimi leo nimekuzaa:

6kama asemavyo mahali pengine,

Wewe u Kuhani milele

Kwa mfano wa daraja la Melkizedeki.

7Yeye siku hizo za niwili wake alimtolea yeye awezae kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa sababu ya kicho chake;

8na, ingawa yu Mwana, alijifunza kutii kwa mateso haya yaliyompata;

9nae alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokofu wa milele kwa watu wote wanaomtii;

10ametajwa na Mungu kuwa Kuhani mkuu kwa mfano wa daraja la Melkizedeki.

11Ambae tuna maneno mengi ya kunena katika khabari zake; na ni shidda kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia.

12Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita) mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu.

13Kwa maana killa mtu atumiae maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.

14Lakini chakula kigumu in cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania