Waebrania 6

Waebrania 6

1KWA sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo illi tuuflkilie utimilifu; tusiweke misingi tena, yaani kuzitubia kazi zisizo na uhayi, na kuwa na imani kwa Mungu,

2na mafundisbo ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele.

3Na tutafanya hayo kama Mungu akitujalia.

4Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,

5na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,

6wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hatta wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu marra ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.

7Maana inchi iinywayo mvua iijiayo marra kwa marra, na kuzaa maboga yejiye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hupokea baraka kwa Mungu;

8bali ikitoa miiba ua magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; mwisho wake ni kuteketea.

9Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika khabari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokofu:

10maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia.

11Nasi twataka killa mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hatta mwisho;

12illi msiwe wavivu, hali wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imaui na uvumilivu.

13Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa kuwa alikuwa hana mkuhwa kuliko nafsi yake wa kumwapia, aliapa kwa nafsi yake,

14akisema, iiakika yangu nitakubariki, na hakika yangu nitakuongeza.

15Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.

16Maana wana Adamu humwapia yeye aliye mkuu: na ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kiyathubutishe.

17Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha wairithio ile ahadi jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati;

18illi kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu bawezi kusema nwongo, tupate faraja lililo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;

19tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo mle mlimo ndani ya pazia,

20alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa Kuhani mkuu kwa jinsi ya Melkizedeki hatta milele.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania