The chat will start when you send the first message.
1NIKAONA ishara nyingine katika mbingu, kubwa, ya ajabu, malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo hasira ya Mungu imetimia.
2Nikaona kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, nao wenye kushinda, na kujiepusha na yule nyama na sanamu yake na alama yake, na hesabu ya jina lake, wamesimama juu ya bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.
3Nao wauimba uimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na uimbo wa Mwana kondoo, wakisema, Makuu, ya ajabu, matendo yako, ee Bwana Mungu Mwenyiezi; za haki, za kweli njia zako, ee Mfalme wa watakatifu.
4Ni nani asiyekucha, Bwana, na kulitukuza jina lako? kwa kuwa wewe peke yako Mtakatifu: kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele yako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.
5Na baada ya haya nikaona, na, tazama, hekalu ya khema ya ushuhuda katika mbingu ilifunguliwa;
6na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakaloka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, kingʼaacho, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu.
7Na mmoja wa wale nyama wane wenye uliayi akawapa vichupa saba vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya Mungu aliye hayi hatta milele na milele.
8Hekalu ikajazwa moshi uliotoka kwa utukufu wa Mungu na uweza wake. Na hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu hatta yatakapotimizwa mapigo saba ya wale malaika saba.