Ufunuo 17

Ufunuo 17

1AKAJA mmoja wa malaika wale saba wenye vile vichupa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi,

2ambae wafaime wa inchi walizini nae, nao wakaao katika inchi wakalevywa kwa mvinyo ya uasharati wake.

3Akanichukua katika Roho hatta jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu va nyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya ukafiri, mwefiye vichwa saba na pembe kumi.

4Na mwanamke yule alikuwa ameliwa nguo ya porfuro, na nyekuudu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, mwenye kikombe cha dhahabu mkononi mwake kilichojawa na machukizo na machafu ya uasharati wake,

5Na katiksi kipaji cha uso wake alikuwa na jina, limeandikwa, SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAILABA NA MACHUKIZO YA INCHI.

6Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.

7Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya nyama amehukuae, mwenye vile vichwa saba na zile pemhe kumi.

8Yule nyama uliyemwona alikuwako, nae hayuko, nae yu tayari kupanda katika abuso na kwenda kwenye uharibifu. Nao wakaao juu ya inchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watataajabu wamwonapo yule nyama, ya kwamba alikuwako, nae hayuko, nae atakuwako.

9Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke yule.

10Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Nae atakapokuja imempasa kukaa muda mchache.

11Na yule nyama aliyekuwako nae hayuko, yeye ndiye wa nane, nae ni mmoja wa wale saba, nae aenenda kwenye uharibifu.

12Na zile pemlbe kumi ulizoziona ni wafalme, ambao hawajaupokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme kwa saa moja pamoja na yule nyama.

13Hawa wana shauri amoj, nao wampa yule nyama nguvu zao na mamlaka yao.

14Hawa watafanya vita na Mwana kondoo, na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; nao walioitwa wateule, waaminifu, watashinda pamoja nae.

15Akaniambia, Yale maji uliyoyaona, aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.

16Na zile pembe kumi ulizoziona juu ya nyama, hao watamchukia yule kahaba, na watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kahisa kwa moto.

17Maana Muugu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule nyama ufalme hatta maneno ya Mungu yatimizwe.

18Na yule mwanamke uliyemwona, ndiye mji ule mkubwa, mwenye ufalme juu ya wafalme wa inchi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania