The chat will start when you send the first message.
1BAADA ya haya nalioua malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu, inchi ikaangazwa kwa utukufu wake.
2Akalia kwa nguvu, kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya killa roho mchafu, na ngome ya killa ndege mchafu mwenye kuchukiza;
3kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasharati wake, na wafalme wa inchi wamezini nae, na matajiri ya inchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.
4Nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
5Kwa maana dhambi zake zimefika hatta mbinguni, na Mungu amekumhuka dhuluma zake.
6Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mardufu kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikomhe kile alichokichanganisha, mchanganishieni mardufu.
7Kwa kadiri aliyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri hiyo hiyo. Kwa kuwa alisema moyoni mwake, Nimeketi malkiya, nami si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.
8Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, manti, na huzuni, na njaa, nae atateketezwa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni hodari.
9Na wafalme wa inchii waliozini nae na kufanya anasa pamoja nae, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuumgua kwake,
10wakisimama mbali kwa khofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole wake mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio hodari kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.
11Na matajiri wa inchi walia na kumwombolezea kwa sababu hapana mtu anunuae bidhaa yake tena,
12bidhaa ya dhahahu, na fedha, na jito lenye thamani, na lulu, na katani, na porfuro, na hariri, na nguo nyekundu; na killa mti wa uudi, na killa chombo cha pembe, na killa chombo cha mti wa thamani nyingi na cha shaba na cha chuma na cha marimari:
13na mdalasini, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na nganu, na ngʼombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wana Adamu.
14Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fakhari vimekuondokea; wala hulaviona tena kamwe.
15Na wafanyi biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwsike, watasimama mbali, kwa khofu yii maumivu yako, wakilia na kuomboleza,
16wakisema, Ole, ole wake mji ule mkuu uliovikwa katani, na porfuro, na nguo nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu na kito cha thamani na lulu;
17kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa. Na killa mshika msukani na killa aendae mahali kwa matanga, mi baharia, nao wote watendao kazi baharini wakasimama mbali,
18wakalia sana, walipouona moshi wa kuungua kwake, wakisema, Ni mji upi ulio mfano wa mji huu mkubwa!
19Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitoka machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole wake mji ule ulio mkuu, ambao ndani yake wote wenye merikebu katika bahari walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.
20Furahini juu yake, enyi mbingu, na ninyi watakatifu na mitume na manabii, kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake.
21Na malaika mmoja hodari akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Hivi kwa nguvu nyingi utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana kabisa.
22Wala sauti ya wapiga vinanda na ya wapiga mazumari na ya wapiga filimbi na ya wapiga baragumu haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala fundi aliye yote wa kazi iliyo yote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa;
23wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa, wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana wafanyi biashara wako walikuwa wakuu wa inchi, kwa kuwa mataifa yote wamedanganywa kwa uchawi wako.
24Na ndani yake ilionekana damu ya manabii na ya watakatifu na ya wale wote waliouawa juu ya inchi.