The chat will start when you send the first message.
1BAADA ya baya nikasikia sauti ya makutano mengi, sauti kubwa katika mbingu, ikisema, Halleluya; Wokofu na utukufu na nguvu zina Bwana Mungu wetu;
2kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki: maana amemhukumu yule kahabu mkuu aliyeiharibu inchi kwa uasharati wake, na kumpatiliza kwa ajili va damu ya watumwa wake mkononi mwake.
3Wakasema marra ya pili, Halleluya. Na moshi wake hupaa juu hatta milele na milele,
4Na wale wazee ishirini na wane, na wale nyama wane wenye uhayi wakasujudu na kumwabudu Mungu aketiye katika kiti cha enzi, wakisema, Amin, Halleluya.
5Sauti ikatoka katika kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumishi wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo na wakuu.
6Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Halleluya; kwa kuwa Bwana Mungu Mwenyiezi amemiliki.
7Na tufurahi tukashangilie tukampe ulukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.
8Nae alipewa kuvikwa kwa katani safi, ya fakhari, kwa maana katani hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
9Akaniambia, Andika, Wa kheri walioitwa kwa karamu ya arusi ya Mwana Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.
10Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.
11Nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama farasi mweupe, nae aliyempanda, aitwae Mwaminifu na wa kweli, nae kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12Na macho yake yalikuwa kama mwako wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi, nae ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu illa yeye mwenyewe.
13Nae amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na, jina lake, aitwa, Neno la Mungu.
14Na majeslii yaliyo mbinguni yakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa katani safi, nyeupe.
15Na upanga mkali hutoka kinywani mwake awapige mataifa kwa huo. Nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, nae anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ukali wa ghadhabu ya Mungu Mwenyiezi.
16Nae ana jina limeandikwa katika vazi lake mi paja vake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.
17Nikaona malaika mmoja amesimama katika jua, akilia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao kati kati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu,
18mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya maakida, na nyama ya watu hodari na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana na watumwa, wadogo na wakubwa.
19Nikamwonu nyama, na wafalme wa inchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, na na majeshi yake.
20Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;
21na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya farasi yule, utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.