The chat will start when you send the first message.
1BAADA ya haya naliona, na tazama mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hatta huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana buddi kuwa baada ya bayo.
2Na marra nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na juu ya kile kiti ameketi mmoja:
3na yeye aliyeketi alikuwa mithili ya jiwe la yaspi na sardio, na upinde wa mvua nlikizunguka kiti kile cha enzi, mithili ya zumaridi.
4Na viti ishirini na vine vilikizuniguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wane, wamekeli, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.
5Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na ngurumo na sauti. Na taa saha za moto zikiwaka mbele ya kiti kile cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.
6Na mliele ya kile kiti cha enzi, mfano wa bahari ya kioo eheupe, kama krustallo, na kati kati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, nyama wane, wamejaa macho mbele na nyuma.
7Na nyama wa kwanza alikuwa mfano wa simba, na nyama wa pili mfano wa ndama, na nyama wa tatu mwenye nso kama uso wa Mwana Adamu, na nyama wa nne mfano wa tai arukae.
8Na hawa nyama wane, wenye uhayi, killa mmoja alikuwa na mabawa sita: pande zote na ndani wamejaa macho, nao hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyiezi, aliyekuwako, nae yuko, nae anakuja.
9Na hawa nyama wenye uhayi watakapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi yeye aliye hayi hatta milele na milele ntukufu na heshima na shukrani,
10ndipo hawa wazee ishirini na wane watakapoanguka mbele zake aketiye juu ya kiti cha enzi, nao watamsujudu veye aliye hayi hatta milele na milele, nao watatupa taji zao mbele ya kiti eha enzi, wakisema,
11Umestahili, Bwana, Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na nweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, vikaumbwa.