Ufunuo 5

Ufunuo 5

1NIKAONA katika mkono wa kuume wa aliyeketi juu ya kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.

2Nikaona malaika mwenye nguvu akikhubiri kwa santi kuu, Nani astahiliye kukifungua kitabu na kuzivunja muhuri zake?

3Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya inchi, wala chini ya inchi, aliyeweza kukifunua kitabu wala kukitazama.

4Nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifuugua kitabu na kukisoma, wala kukitazama.

5Na mmoja wa wale wazee akaniambia, Usilie, tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, shina la Daud, yeye amepata uwezo wa kukifunua kitabu na kuzivunja zile muhuri saba.

6Nikaona, na tazama, kati kati ya kiti cha enzi na ya nyama wane wenye uhayi, na kati kati ya wale wazee, Mwana Kondoo, amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.

7Akaja, akakitwaa kitabu katika mkono wa kuume wake aliyeketi juu ya kiti kile cha enzi.

8Hatta alipokitwaa kile kitabu, nyama wane wenye uhayi na wale wazee ishirini na wane wakaanguka mbele ya Mwana Kondoo, killa mmoja wao ana kinubi, na vitupa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambavyo ni maombi ya watakatifu.

9Nao waimba uimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulicbinjwa

10ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa killa kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu: nao wanamiliki juu ya inchi.

11Nikaona, nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale nyama wenye uhayi, na za wale wazee, na hesabu yao, elfu kumi marra elfu kumi, na elfu marra elfu,

12wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana Kondoo aliyechinjwa kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.

13Na killa kiumbe kilicho mbinguni na juu ya inchi na chini ya inchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na una Mwana Kondoo hatta milele na milele.

14Na wale nyama wane wenye uhayi wakasema, Amin. Na wale wazee ishirini na wane wakaanguka wakamsujudu yeye aliye hayi milele na milele.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania