The chat will start when you send the first message.
1NIKAONA hapo Mwana Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri, nikasikia mmoja wa wale nyama wenye uhayi akisema, kama sauti ya ngurumo, Njoo! uone.
2Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana upinde, akapewa taji, akatoka, akishinda na apate kushinda.
3Na alipofungua muhuri ya pili, nikamsikia nyama wa pili akisema, Njoo uone.
4Akatoka farasi mwingine mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katikii inchi, watu wauawe, akapewa upanga mkubwa.
5Na alipoifungua muhuri ya tatu nikamsikia nyama wa tatu mwenye uhayi akisema, Njoo, none. Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.
6Nikasikia sauti kati kati ya nyama wane wenye uhayi, ikisema, Kibaba cha nganu kwa nussu rupia, na vibaba vitatu vya shairi kwa nussu rupia, wala usiyadhuru mafuta na mvinyo.
7Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya nyama wa nne akisema, Njoo uone.
8Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Manti, na Kuzimu akafuatana nae. Wakapewa mamlaka juu ya robo ya inchi wane kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa nyama mwitu wa inchi.
9Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhbahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.
10Wakalia kwa sauti kuu, wakiseina, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hatta lini huhukumu na kuipatia haki damu yetu kwao wakaao juu ya inchi?
11Wakapewa killa mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hatta itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao watakaouawa vile vile kama wao.
12Nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, tazama, palikuwa tetemeko kuu la inchi, jua likawa jeusi kama gunia la nywele, mwezi ukawa kama damu,
13nyota zikaanguka juu ya inchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14Mbingu zikaondolewa kaina ukarasa uliokunjwa, na killa mlima na kisiwa vikahamishwa katika mahali pake.
15Na wafalme wa dunia, na wakuu, na matajiri, na majemadari, na wenye nguvu, na killa mtumwa, na mungwana, wakajificha katika pango za chini ya miamba ya milima,
16wakaiambia milima na miamba, Tuangukieni, katusetirini, tusione uso wake aketiye juu ya kiti cha enzi wala hasira ya Mwana Kondoo.
17Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yake, imekuja: na nani awezae kusimama?