Ufunuo 7

Ufunuo 7

1BAADA ya haya nikaona malaika wane wamesimama katika pembe nne za inchi, wakizizuia pepo nne za inchi, upepo usivume juu ya inchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.

2Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hayi: akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wane waliopewa kuidhuru inchi na bahari,

3akisema, Msiidhuru inchi wala bahari wala miti hatta tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mwenyiezi Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao.

4Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika killa kabila ya wana wa Israeli, watu mia na arubaini na nne elfu.

5Wa kabila ya Yuda thenashara elfu waliotiwra muhuri.

Wa kabila ya Reuben thenashara elfu.

Wa kabila ya Gad thenashara elfu.

Wa kablia ya Asher thenashara elfu.

6Wa kabila ya Naftali thenashara elfu.

Wa kaliila ya Manasse thenashara elfu.

7Wa kabila ya Sumeon thenashara elfu.

Wa kabila ya Lawi thenashara elfu.

Wa kabila ya Issakar thenashara elfu.

8Wa kabila ya Zabulon thenashara elfu.

Wa kabila ya Yusuf thenashara elfu.

Wa kabila ya Benyamin thenashara elfu waliotiwa muhuri.

9Baada ya haya nikaona, na tazama mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezae kuuhesabu, watu wa killa taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kiti kile cha enzi, na mbele za Mwana Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;

10wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokofu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana Kondoo.

11Na malaika wote wamesimama pande zote za kiti cha enzi na za wazee na za vile viumbe vine vyenye uhayi, wakaanguka kifudifudi mbele ya kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,

12wakisema, Amin: Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu milele na milele. Amin.

13Akajibu mmoja wa wale wazee akaniambia, Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni nani? na walikotoka wapi?

14Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hawo ndio wanaotoka katika shidda ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao wakayafanya meupe katika damu ya Mwana Kondoo.

15Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda khema yake juu yao.

16Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote.

17Kwa maana Mwana Kondoo aliye kati kati ya kiti cha enzi atawachunga, nae atawaongoza kwenye chemcheni za inaji yenye uhayi, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania