The chat will start when you send the first message.
1BASSI, tusemeje? Ibrahimu baba yetu kwa jinsi ya mwili amepata nini?
2Kwa maana ikiwa Ibrahimu alipewa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia, lakini si mbele za Mungu.
3Maana maandiko yasemaje? Ibrabimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.
4Lakini kwa mtu afanyae kazi ujira wake hauhesabiwi kuwa neema bali kuwa deni.
5Lakini kwa mtu asiofanya kazi, bali anamwammi yeye ampae haki asiye mtawa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.
6Kama vile Daud aunenavyo ukheri wake mtu yule ambae Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo;
7Wa kheri waliosamehewa maasi yao,
Na waliosetiriwa dhambi zao.
8Yu kheri mtu yule ambae Bwana hamhesabii dhambi.
9Bassi ukheri huu ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba Ibrahimu kwa ajili ya imani yake aliliesabiwa wema.
10Alihesabiwaje bassi? Alipokwisha kutahiriwa, au kabla hajatahiriwa? Si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa.
11Nae aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya wema wa imani aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, illi na wao pia wahesahiwe wema;
12na baba ya kutahiriwa, si kwa hao waliotahiriwa tu, bali kwa hao waliotahiriwa na kuzifuasa uyayo za imani yake baba yetu Ibrahimu aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa.
13Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sharia bali kwa wema aliopata kwa imani.
14Maana ikiwa wale wa sharia ndio warithi, imani imekuwa burre, na ahadi imebatilika.
15Kwa sababu sharia ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipo sharia, hapana kosa.
16Kwa hiyo ilitoka kwa imani, iwe kwa njia ya neema, illi ile ahadi iwe imara kwa wazao wote, si kwa wale wa torati tu, illa na kwa wale wa imani ya Ibrahimu aliye baba yetu sisi sote,
17(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi) mbele zake aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, avitajae vitu visivyokuwa kana kwamba vimekuwa.
18Ambae aliamini kwa kutazamia yasiyoweza kutazamiwa, kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa nzao wako.
19Asiyekuwa dhaifu wa imani, wala hakutia moyoni hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa (akiwa amekwisha kupata miaka mia), wala hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
20Wala hakuionea shaka ahadi ya Mungu kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani yake, akimtukuza Mungu,
21akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
22Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa haki.
23Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake,
24bali na kwa ajili yetu sisi tutakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu katika wafu, Bwana wetu,
25aliyetolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa illi tupate kupewa haki.