The chat will start when you send the first message.
1BASSI tukiisha kuhesabiwa wema utokao katika imani, tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo;
2kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; na twafurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.
3Wala si hivyo tu, illa twafurahi katika mateso pia, tukijua ya kuwa dhiiki, kazi yake ni kuleta uvumilivu,
4na kazi ya uvumilivu uthabiti wa moyo, na kazi ya uthabiti wa moyo tumaini,
5na tumaini halitahayarishi, kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepcwa sisi.
6Kwa maana hapo tulipokuwa sisi hatuna nguvu, wakali ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya maasi.
7Kwa maana ni shidda mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki, illakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema.
8Bali Mungu aonyesha pendo lake kwetu, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
9Bassi zaidi sana tukiisha kupewa haki katika damu yake tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
10Kwa maana tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.
11Wala si hivyo tu, illa na twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambae kwa yeye tuliupokea upatanisho.
12Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote;
13kwa maana wote wamefanya dhambi; maana kabla ya sharia dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi sharia isipokuwapo;
14lakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hatta wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu aliye mfano wake yeye atakaekuja.
15Lakini kipawa kile hakikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kuanguka kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema ya mtu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.
16Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyekosa si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu, bali kipawa cha neema kilikuja kwa ajili ya makosa mengi, kikaleta kuachiliwa.
17Kwa maana ikiwa kwa kuteleza mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.
18Bassi tena, kama vile kwa anguko moja watu wote walihukumiwa, vivyo hivyo kwa tendo moja la haki watu wote walipewa haki yenye uzima.
19Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wote waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, vivyo hivyo kwa kutii kwake mtu mmoja watu wote wameingizwa katika hali ya wenye haki.
20Sharia iliingia illi anguko lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;
21illi, kama vile dhambi ilivyotawaia katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hatta uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.