The chat will start when you send the first message.
1Wote ambao ni watumwa waoneshe heshima kubwa kwa mabwana zao. Ndipo jina la Mungu na mafundisho yetu hayatakosolewa.
2Baadhi ya watumwa wanao mabwana ambao ni waamini, hivyo hao ni ndugu. Je! inamaanisha wasiwaheshimu mabwana zao? Hapana, watawatumikia hata kwa uzuri zaidi, kwa sababu wanawasaidia waaminio, watu wawapende.
Haya ni mambo ambayo lazima uyafundishe na kumwambia kila mtu kufanya.
3Watu wengine wanafundisha uongo na hawakubaliani na mafundisho ya kweli ambayo yanatoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Hawakubali mafundisho ambayo yanatuongoza kumheshimu na kumpendeza Mungu.
4Wanajivunia wanayoyafahamu, lakini hawaelewi chochote. Wamepagawa na wana ugonjwa wa kupenda mabishano na mapigano ya maneno. Na hayo yanaleta wivu, ugomvi, matusi, na uovu wa kutoaminiana.
5Daima wanaleta shida, kwa sababu ni watu ambao kufikiri kwao kumeharibiwa. Wamepoteza ufahamu wao wa ukweli. Wanafikiri kwamba kujifanya wanamheshimu Mungu ni njia ya kupata utajiri.
6Kuishi kwa kumheshimu Mungu, hakika, ni njia ambayo watu hutajirika sana, kwa sababu inamaanisha wanaridhika na walivyo navyo.
7Tulipokuja ulimwenguni, tulikuja bila kitu, na tutakapokufa hatutachukua chochote.
8Hivyo, kama tukiwa na chakula na nguo, tutaridhika navyo.
9Watu ambao wanatamani kuwa matajiri wanajiletea majaribu wenyewe. Wananasa katika mtego. Wanaanza kutaka vitu vingi vya kijinga ambavyo vitawaumiza na kuwaharibu.
10Kupenda fedha kunasababisha aina zote za uovu. Watu wengine wamegeuka kutoka kwenye imani yetu kwa sababu wanataka kupata fedha nyingi zaidi. Lakini wamejisababishia wenyewe maumivu mengi na huzuni.
11Lakini wewe ni mali ya Mungu. Hivyo kaa mbali na mambo hayo yote, daima jaribu kutenda mema ili umheshimu Mungu na uwe na imani, upendo, uvumilivu, na upole.
12Tunatakiwa tupigane kutunza imani yetu. Jaribu kwa bidii kadri unavyoweza kushinda vita vya thawabu. Tunza uzima wa milele. Ni uzima mliyouchagua kuupata mlipoikiri imani yenu katika Yesu; huo ukweli wa ajabu mliousema waziwazi kwa wote kuusikia.
13Mbele ya Mungu na Kristo Yesu nakupa amri. Yesu ni yule aliyeshuhudia ukweli aliposimama mbele ya Pontio Pilato. Mungu ndiye anayetoa uhai kwa kila kitu. Nakuambia haya sasa:
14Tenda niliyokuamuru kufanya bila dosari au kulaumu mpaka muda atakapo rudi.
15Mungu atafanya hayo yatokee wakati utakapotimia. Yeye ni mwenye utukufu zaidi na mtawala pekee, mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.
16Mungu pekee hafi, anaishi katika nuru angavu sana ambayo watu hawawezi kusogea karibu. Hakuna mtu aliyemwona Mungu; wala anayeweza kumuona. Heshima na nguvu ni zake milele. Amina.
17Wape amri hii wale ambao ni matajiri wa vitu vya ulimwengu huu. Waambie wasiwe na majivuno, bali wamtumaini Mungu wala si katika fedha zao. Fedha haziwezi kuaminiwa, lakini Mungu anatuhudumia kwa ukarimu mkubwa na anatupa vitu vyote ili tufurahi.
18Waambie wale ambao ni matajiri watende mema. Wawe matajiri katika kuzifanya kazi njema. Na uwambie wawe tayari kutoa na kuwapa wengine vitu.
19Kwa kufanya hivi, watajiwekea hazina kwa ajili yao wenyewe. Na hazina hiyo itakuwa ni msingi imara huo utakuwa msingi imara ambao maisha yao ya siku zinazokuja yatajengwa. Wataweza kuwa na maisha yaliyo ya kweli kabisa.
20Timotheo, Mungu ameweka vitu vingi kwako uvitunze. Uvitunze vyema. Jitenge na watu wanaosema mambo yasiyofaa ambayo hayatoki kwa Mungu na wale wanaokupinga na “elimu” ambayo siyo “elimu” kabisa.
21Watu wengine wanaodai kuwa na “elimu” wamepotea mbali kabisa kutokana na wanachoamini.
Ninaomba neema ya Mungu iwe kwenu nyote.