The chat will start when you send the first message.
1Ndipo nikaona ajabu nyingine mbinguni, ilikuwa kubwa na ya kushangaza. Walikuwepo malaika saba wenye mapigo saba. Haya ni mapigo ya mwisho kwa sababu baada ya haya, ghadhabu ya Mungu itakuwa imekwisha.
2Niliona kama bahari ya kioo iliyochanganyikana na moto. Wale wote waliomshinda mnyama na sanamu yake na namba ya jina lake walikuwa wamesimama kando ya bahari. Watu hawa walikuwa na vinubi walivyopewa na Mungu.
3Waliuimba wimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu na wimbo wa Mwanakondoo:
“Mambo unayotenda ni makuu na ya kushangaza,
Bwana Mungu Mwenye Nguvu.
Njia zako ni sahihi na za kweli,
mtawala wa mataifa.
4Watu wote watakucha wewe, Ee Bwana.
Watu wote watalisifu jina lako.
Mtakatifu ni wewe peke yako.
Watu wote watakuja na kusujudu mbele yako,
kwa sababu ni dhahiri kuwa wewe hutenda yaliyo haki.”
5Baada ya hili nikaona hekalu, mahali patakatifu pa Mungu mbinguni. Likiwa wazi;[#15:5 Kwa maana ya kawaida, “Hema ya Ushuhuda”. Tazama katika Orodha ya Maneno. Tazama Kut 25:8-22.]
6kisha malaika saba wenye mapigo saba wakatoka nje ya hekalu. Walikuwa wamevaa kitani safi inayong'aa. Wamevaa mikanda mipana ya dhahabu vifuani mwao.
7Kisha mmoja wa viumbe wenye uhai wanne akawapa malaika bakuli saba za dhahabu. Bakuli zilikuwa zimejaa ghadhabu ya Mungu, aishiye milele na milele.
8Hekalu lilikuwa limejaa moshi uliotoka katika utukufu na nguvu ya Mungu. Hakuna ambaye angeweza kuingia hekaluni mpaka mapigo saba ya malaika saba yamemalizika.