1 Mambo 24

Mafungu 24 ya watambikaji.

1Mafungu yao wana wa Haroni ni haya: wana wa Haroni walikuwa Nadabu na Abihu, Elazari na Itamari.[#1 Mambo 6:3; 23:6.]

2Nadabu na Abihu wakafa, baba yao akingalo yupo, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo Elazari na Itamari wakaupata utambikaji.[#3 Mose 10:1-2,12.]

3Dawidi akapatana na Sadoki aliyekuwa wa wana wa Elazari na Ahimeleki aliyekuwa wa wana wa Itamari, akawagawanya, kama walivyokuwa na ukuu katika utumishi wao.[#2 Mambo 8:14.]

4Hapo ikatokea, ya kuwa wana wa Elazari walikuwa wenye wakuu wengi zaidi kuliko wana wa Itamari; kwa hiyo walipowagawanya, wakatokea kwa wana wa Elazari wakuu wa milango kumi na sita, lakini kwa wana wa Itamari wakuu wa milango wanane tu.

5Lakini wao kwa wao wakawagawanya kwa kuwapigia kura, kwani walikuwako watambikaji wakuu wa Patakatifu na watambikaji wakuu wa Mungu kwao wana wa Elazari nako kwao wana wa Itamari.

6Naye Semaya, mwana wa Netaneli, aliyekuwa mwandishi wao Walawi akawaandika, mfalme na wakuu wake na mtambikaji Sadoki na Ahimeleki, mwana wa Abiatari, na wakuu wa milango ya watambikaji na Walawi wakitazama, ikawa hivi: mlango mmoja wa Elazari ukichukuliwa kwa kura, ukachukuliwa nao wa pili, kisha ukachukuliwa nao mmoja wa Itamari.[#1 Mambo 18:16.]

7Kura ya kwanza ikamwangukia Yoyaribu, ya 2 Yedaya,

8ya 3 Harimu, ya 4 Seorimu,

9ya 5 Malkia, ya 6 Miyamini,

10ya 7 Hakosi, ya 8 Abia,[#Luk. 1:5.]

11ya 9 Yesua, ya 10 Sekania,

12ya 11 Eliasibu, ya 12 Yakimu,

13ya 13 Hupa, ya 14 Yesebabu,

14ya 15 Bilga, ya 16 Imeri,

15ya 17 Heziri, ya 18 Hapisesi,

16ya 19 Petaya, ya 20 Ezekieli,

17ya 21 Yakini, ya 22 Gamuli,

18ya 23 Delaya, ya 24 Mazia.

19Huu ulikuwa ukuu wao katika utumishi wao wa kuingia nyumbani mwa Bwana kwa matengenezo yao, aliyoyatoa baba yao Haroni, kama Bwana Mungu wa Isiraeli alivyomwagiza.

Wakuu wa Walawi.

20Wale wana wengine wa Lawi ni hawa: Kwa wana wa Amuramu: Subaeli, kwa wana wa Subaeli: Yehedia.

21Kwake Rehabia: wana wa Rehabia mkuu wao alikuwa Isia.[#1 Mambo 23:17-23; 26:25.]

22Kwao wa Isihari: Selomoti, kwa wana wa Selomoti: Yahati.

23Nao wana wa Heburoni walikuwa Yeria, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, wa nne Yekamamu.

24Wana wa Uzieli ni Mika, kwa wana wa Mika: Samiri.

25Ndugu ya Mika alikuwa Isia, kwa wana wa Isia alikuwa Zakaria.

26Wana wa Merari walikuwa: Mahali na Musi na wana wa Mwanawe Yazia.

27Wana wa Merari waliokuwa wa mwanawe Yazia ndio Sohamu na Zakuri na Iburi.

28Wa Mahali alikuwa Elazari asiyekuwa na wana.

29Wa Kisi ndio wana wa Kisi: Yerameli.

30Wana wa Musi walikuwa Mahali na Ederi na Yerimoti. Hawa ndio wana wa Lawi kwa milango yao.

31Wao nao waliwapigia kura sawasawa kama ndugu zao wana wa Haroni, mfalme Dawidi na Sadoki na Ahimeleki na wakuu wa milango ya watambikaji na Walawi wakitazama; aliyekuwa mkuu wa mlango alipigiwa kura sawasawa kama ndugu yake mdogo.[#1 Mambo 25:8.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania