1 Mambo 4

Vizazi vya Yuda.

1Wana wa Yuda: Peresi, Hesironi na Karmi na Huri na sobali.[#1 Mambo 2:4-5,7,19,50.]

2Naye Raya, mwana wa Sobali, akamzaa Yahati; naye Yahati akamzaa Ahumai na Lahadi. Huu ndio ukoo wao Wasorati.[#1 Mambo 2:53.]

3Hawa ndio wana wa babake Etamu: Izireeli na Isima na Idibasi, nalo jina la umbu lao ni Hasilelponi.

4Tena Penueli, babake Gedori, na Ezeri, babake Husa; hawa ndio wana wa Huri, mwana wa kwanza wa Efurata, babake Beti-Lehemu.[#1 Mambo 2:19,50.]

5Naye Ashuri, babake Tekoa, alikuwa na wanawake wawili: Hela na Nara.

6Nara akamzalia Ahuzamu na Heferi na Temuni na Ahastari. Hawa ndio wana wa Nara.

7Nao wana wa Hela: Sereti, Isihari na Etinani.

8Kosi akamzaa Anubu na Sobeba nao ukoo wa Ahariheli, mwana wa Harumu:

9Yabesi alikuwa mwenye macheo kuliko ndugu zake, naye mama yake akamwita jina lake Yabesi kwamba: Nimemzaa kwa maumivu.

10Naye Yabesi akamwomba Mungu wa Isiraeli kwamba: Laiti ungenibariki sana na kuipanua mipaka yangu, mkono wako ukawa pamoja nami, ukanizuilia mabaya, maumivu yasinipate! Mungu akayatimiza aliyoyaomba.

11Naye Kelubu, ndugu yake Suha, akamzaa Mehiri, ndiye babake Estoni.

12Naye Estoni akamzaa Beti-Rafa na Pasea na Tehina, babake Iri-Nahasi. Hawa ndio wana waume wa Reka.

13Nao wana wa Kenazi: otinieli na Seraya; nao wana wa Otinieli: Hatati.[#Yos. 15:17; Amu. 1:13.]

14Naye Meonotai akamzaa Ofura. Naye Seraya akamzaa Yoabu, babake Ge-Harasimu (Bonde la Wahunzi), kwani walikuwa wahunzi.

15Nao wana wa Kalebu, mwana wa Yefune: Iru, Ela na Namu; nao wana wa Ela: Kenazi.[#4 Mose 13:6; 14:16.]

16Nao wana wa Yehaleleli: Zifu na Zifa, Tiria na Asareli.

17Nao wana wa Ezera: Yeteri na Meredi na Eferi na Yaloni. (Bitia) akachukua mimba ya Miriamu na ya Samai na ya Isiba, babake Estemoa.

18Naye mkewe wa Kiyuda wa Meredi akamzaa Yeredi, babake Gedori, na Heberi, babake Soko, na Yekutieli, babake Zanoa; lakini wale walikuwa wana wa Bitia, binti Farao, Meredi aliyemchukua, awe mkewe.

19Nao wana wa mkewe Hodia, umbu lake Nahamu, babake Keila: Mgarmi na Estemoa wa Maka.

20Nao wana wa Simoni: Amunoni na Rina, Beni-Hanani na Tiloni. Nao wana wa Isi: zoheti na Beni-Zoheti.

21Wana wa Sela, mwana wa Yuda: Eri, babake Leka, na Lada, babake Maresa, nao ukoo wao waliojua kufuma bafta wa mlango wa Asibea;[#1 Mambo 2:3.]

22tena Yokimu na wana waume wa Kozeba na Yoasi na Sarafu waliotawala Moabu, na Yasubi-Lehemu. Lakini maneno haya ni ya kale.

23Hawa ndio wafinyanzi na wenyeji wa Netaimu na wa Gedera; walikaa huko kwa mfalme na kumfanyia kazi.

Vizazi vya Simeoni.

24Wana wa Simeoni: Nemueli na Yamini, Yaribu, Zera, Sauli.[#1 Mose 46:10.]

25Mwanawe alikuwa Salumu, mwanaswe alikuwa Mibusamu, mwanawe alikuwa Misima.

26Nao wana wa Misima: Mwanawe alikuwa Hamueli, mwanawe alikuwa Zakuri, mwanawe alikuwa Simei.

27Naye Simei alikuwa mwenye wana wa kiume kumi na sita na wana wa kike sita, lakini ndugu zake hawakuwa na wana wengi, nao ukoo wao wote haukupata watu wengi kama wana wa Yuda.

28Nao walikaa Beri-Seba na Molada na Hasari-Suali,

29na Biliha na Esemu na Toladi,[#Yos. 19:2-8.]

30na Betueli na Horma na Siklagi,

31na Beti-Markaboti na Hasari-Susimu na Beti-Biri na Saraimu. Hii ndiyo miji yao, mpaka Dawidi aliposhika ufalme.

32Navyo vijiji vyao vilikuwa Etamu na Aini, Rimoni na Tokeni na Asani, ni miji mitano.

33Navyo vijiji vyao vyote vilivyoizunguka miji hii mpaka Baali vilikuwa makao yao, navyo vilikuwa na vitabu vyao vya udugu.

34Tena: Mesobabu na Yamuleki na Yosa, mwana wa Amasiya,

35na Yoeli na Yehu, mwana wa Yosibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli;

36na Eliyoenai na Yakoba na Yesohaya na Asaya na Adieli na Yesimieli na Benaya,

37na Ziza, mwana wa Sifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Simuri, mwana wa Semaya.

38Hawa waliotajwa kwa majina walikuwa wakuu katika ukoo wao, milango ya baba zao ilipokwisha kusambaa kwa wingi.

39Wakaenda, hata waingie Gedori upande wa maawioni kwa jua wa huko bondeni kuwatafutia mbuzi na kondoo wao malisho.

40Wakaona malisho mema ya kuwanonesha, nayo ile nchi ilikuwa pana pande zote, tena ilikuwa yenye utulivu na utengemano, kwani kale watu wa Hamu walikuwa wakikaa huko.[#Amu. 18:7.]

41Wao walioandikwa majina hapo waliingia huko siku zake Hizikia, mfalme wa Yuda, wakayapiga mahema yao pamoja na Wameuni walioonekana huko, wakawatia mwiko wa kuwapo mpaka siku hii ya leo, wakakaa mahali pao, kwani malisho ya mbuzi na kondoo wao yalikuwapo.[#2 Fal. 18:1.]

42Nao wengine wao waliokuwa wana wa Simeoni walikwenda milimani kwa Seiri, watu 500, nao wakuu wao walikuwa Pelatia na Naria na Refaya na Uzieli, wana wa Isi.

43Wakayapiga masao ya Waamaleki walioponea huko, wakakaa huko mpaka siku hii ya leo.[#1 Sam. 15:3,8.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania