The chat will start when you send the first message.
1Mimi Paulo niliyeitwa kuwa mtume wa Kristo Yesu kwa hayo, Mungu ayatakayo, na ndugu Sostene[#1 Kor. 6:11; Tume. 9:14.]
2tunawaandikia ninyi wateule wa Mungu mlioko Korinto; mlitakaswa na Kristo Yesu, mkaitwa kuwa watakatifu pamoja na wote wanaolitambikia Jina la Bwana wetu Yesu Kristo ko kote, huko kwao nako huku kwetu.
3Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo![#Rom. 1:7.]
4*Nayavumisha siku zote mema yake Mungu, aliyowagawia ninyi, mwe katika Kristo Yesu.
5Kwa hivyo, mnavyomkalia, mwazipata mali zote zilizomo katika ufundisho na katika utambuzi wote;
6nao ushuhuda wa Kristo ukapata nguvu kwenu.
7Kwa sababu hii hakuna gawio, mnalolikosa mkiwa mnangoja, Bwana wetu Yesu Kristo atokee waziwazi.[#Tit. 2:13.]
8Yeye ndiye atakayewatia nguvu mpaka mwisho, mpate kutokea siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo mkiwa hamnayo ya kuwakamia.[#Fil. 1:6,10; 1 Tes. 3:13; 5:3.]
9Mungu ni mwelekevu aliyewaita kuwa wenziwe Mwana wake Yesu Kristo aliye Bwana wetu.*[#1 Tes. 5:24.]
10Lakini nawaonya, ndugu, kwa ajili ya Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, wote mseme mamoja, kwenu kusiwe na matengano, ila nguvu yenu iwe ile ya kutenda moyo mmoja na kutambua neno moja tu.[#Fil. 2; 3:6.]
11Kwani ndugu zangu, nimeambiwa mambo yenu na wale wa Kloe, ya kuwa kwenu yako magomvi.
12Nalisema lile la kwamba: Kwenu kila mmoja husema: Mimi wa Paulo! au: Mimi wa Apolo! au: Mimi wa Kefa! au: Mimi wa Kristo! Je?[#1 Kor. 3; Yoh. 1:2; Tume. 18:24,27.]
13Kristo amegawanyika? Au ni Paulo aliyewambwa msalabani kwa ajili yenu? Au mmebatiziwa jila la Paulo?
14Namshukuru Mungu, ya kuwa sikubatiza mtu kwenu ila Krispo na Gayo,[#Tume. 18; Rom. 16:23.]
15maana mtu asiseme: Mmebatiziwa jina langu mimi.
16Kweli naliwabatiza nao wa nyumbani mwa Stefana. Tena sijui, kama yuko mwingine, niliyembatiza.[#1 Kor. 16:5,17.]
17Kwani Kristo hakunituma kubatiza, ila amenituma kuipiga hiyo mbiu njema, lakini si kwa maneno ya ujuzi wa kimtu, msalaba wake Kristo usitenguliwe.[#1 Kor. 2:4; Mat. 28:9; 28:19; Yoh. 4:2.]
18Kwani neno la kuwambwa msalabani ndilo la upuzi kwao wanaoangamia, lakini kwetu sisi tunaookolewa ndilo la nguvu ya Mungu.[#Rom. 1:16; 2 Kor. 4:3.]
19Kwani imendikwa:
Nitauangamiza werevu wao walio werevu wa kweli
nao utambuzi wao watambuzi.
20Yuko wapi aliye mwerevu wa kweli? Yuko wapi aliye mwandishi? Yuko wapi aliye mbishi wa siku hizi? Je? Mungu hakuupumbaza werevu wa ulimwengu huu?[#Iy. 12:17.]
21*Kwani kwa huo werevu wake ulimwengu huu haukumtambua Mungu na werevu wake wa Kimungu ulio wa kweli; kwa hiyo Mungu amependezwa kuwaokoa wenye kumtegemea akiwatangazia mapumbavupumbavu.[#Mat. 11:25.]
22Kwani Wayuda hutaka vielekezo, nao Wagriki hutafuta werevu ulio wa kweli.[#Mat. 12:38; Yoh. 4:48; Tume. 17:18,32.]
23Lakini sisi twamtangaza Kristo, alivyowambwa msalabani; ndipo, Wayuda wajikwaliapo, tena ndipo, wamizimu waoneapo mapumbavu tu.[#1 Kor. 2:14; Rom. 9:32; Gal. 5:11; 6:12.]
24Lakini wale walioitwa, Wayuda na Wagriki, kwao twamtangaza Kristo kwamba: Ni nguvu ya Mungu, tena: Ni werevu wa Mungu ulio wa kweli.[#1 Kor. 1:18; Kol. 2:3.]
25Kwani yaliyo mapumbavu ya Mungu ndiyo yenye werevu wa kweli kuupita wa watu, nayo yaliyo manyonge ya Mungu ndiyo yenye nguvu kuzipita za watu.
26Kwani utazameni, ndugu, wito wenu! Hakuna wengi walio werevu wa kimtu; hakuna wengi walio wenye nguvu; hakuna wengi walio wenye macheo.[#Mat. 11:25; Yoh. 7:48; Yak. 2:1-5.]
27Lakini walio wapumbavu wa ulimwengu huu ndio, Mungu aliowachagua, awatweze walio werevu wa kweli. Tena walio wanyonge wa ulimwengu huu ndio, Mungu aliowachagua, awatweze wenye nguvu.
28Tena walio wakiwa wa ulimwengu huu nao waliobezwa ndio, Mungu aliowachagua, hata wasiowaziwa kuwa watu, awaumbue wanaotukuzwa kwamba: Ni watu,[#Luk. 1:52-53.]
29kusudi mbele ya Mungu mwenye mwili wa kimtu asijivune, hata mmoja.[#Rom. 3:27; Ef. 2:9.]
30Kwake yeye ndio, mlikotoka ninyi mliomo mwake Kristo Yesu. Huyu ndiye werevu wetu wa Kimungu ulio wa kweli, na wongufu na utakasi na ukombozi.[#Yer. 23:5-6; Mat. 20:28; Yoh. 17:19; 2 Kor. 5:21.]
31Basi, iwe, kama ilivyoandikwa:
Mwenye kujivuna na ajivunie kuwa wa Bwana!*