The chat will start when you send the first message.
1*Ndugu, sitaki, ninyi mkose kujua, ya kuwa baba zetu wote walikwenda wakifunikwa na wingu, nao wote walipita baharini.[#2 Mose 13:21; 14:22.]
2Wote wakabatiziwa Mose walipokuwa winguni na baharini.
3Tena chakula cha Kiroho, walichokila wote, ni kile kimoja;[#2 Mose 16:4,35; 5 Mose 8:3.]
4nacho kinywaji cha Kiroho, walichokinywa wote, ni kile kimoja. Maana walikunywa maji yaliyotoka katika mwamba wa Kiroho uliofuatana nao; nao mwamba huo ni Kristo.[#2 Mose 17:6.]
5Lakini wale wengi Mungu hakupendezwa nao, kwa hiyo walilazwa jangwani.[#4 Mose 14:23,36.]
6Hayo yalifanyika, tujifunzie mumo humo, sisi tusitende tamaa ya maovu, kama wale walivyokuwa na tamaa.[#4 Mose 11:4,34.]
7Wala msitambikie kinyago kama wengine wao! Kama ilivyoandikwa:
Watu walikalia kula na kunywa,
kisha wakainukia kucheza.
8Tena tusifanye ugoni, kama wengine wao walivyoufanya, wakauawa siku moja watu 23000.[#4 Mose 25:1,9.]
9Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaangamizwa na nyoka.[#4 Mose 21:4-6.]
10Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaangamizwa na mwangamizaji.[#4 Mose 14:2,36; Ebr. 3:11,17.]
11Lakini hayo yote yaliwapata, tujifunzie mumo humo, yakaandikiwa kutuonya sisi tuliofika penye mwisho wa siku.
12Kwa hiyo: ajiwaziaye kwamba amesimama, aangalie, asianguke!
13Hamjaingiwa bado na jaribu lo lote linaloipita nguvu ya mtu. Lakini Mungu ni mwelekevu; hatawaacha ninyi, mjaribiwe na mambo yaupitayo uwezo wenu; lakini hapo, mtakapojaribiwa, atawapatia mzungu, mweze kuvumilia.*
14Kwa hiyo, wenzangu wapendwa, yakimbieni matambiko ya mizimu![#1 Yoh. 5:21.]
15Nasema nanyi, kwa kuwa m wenye akili; yatambueni ninyi, niyasemayo!
16Kinyweo chenye mbaraka, tukibarikicho, hakitupatii bia ya damu yake Kristo? Mkate, tuumegao, hautupatii bia ya mwili wake Kristo?[#1 Kor. 11:23-25; Mat. 26:27; Tume. 2:42.]
17Kwa sababu mkate ni mmoja, nasi tulio wengi tu mwili mmoja, maana sote twagawiwa huo mkate mmoja.*[#1 Kor. 12:27; Rom. 12:5.]
18Mwatazame walio Waisiraeli kwa kuzaliwa! Wenye kuzila nyama za tambiko sio wenye bia ya meza ya kutambikia?[#3 Mose 7:6,15.]
19Basi, nisemeje? Niseme: Nyama ya tambiko ni kitu? Au niseme: Mizimu ni kitu?[#1 Kor. 8:4.]
20Siyo, maana wamizimu waitambikia mizimu yao, hawamtambikii Mungu. Nami sitaki, ninyi mwe wenye bia na mizimu.[#3 Mose 17:7; 5 Mose 32:17; Sh. 106:37; Ufu. 9:20.]
21Hamwezi kukinywa kinyweo cha Bwana nacho kinyweo cha mizimu; hamwezi kula mezani pa Bwana na mezani pa mizimu.
22Au tumchokoze Bwana? Sisi tuko na nguvu kumshinda yeye?[#2 Kor. 6:15-16.]
23Hakuna cho chote chenye mwiko, lakini sivyo vyote vifaavyo; hakuna cho chote chenye mwiko, lakini sivyo vyote vijengavyo.[#1 Kor. 6:12.]
24Pasiwe na mtu mwenye kuyatafuta yaliyo yake, sharti ayatafute yaliyo ya mwenziwe![#1 Kor. 10:33; Rom. 15:2.]
25Vyote vinavyouzwa sokoni vileni pasipo kuuliza vitokapo, mioyo isilemewe![#Rom. 14:2-10,22.]
26Kwani nchi hii ni yake Bwana navyo vyote vilivyomo.[#Sh. 24:1.]
27Mtu asiyemtegemea Mungu akiwaalika, nanyi mkitaka kwenda, basi, vyote mnavyoandaliwa vileni pasipo kuuliza vitokapo mioyo isilemewe!
28Lakini akiwaambia: Hii ni nyama ya tambiko, msiile kwa ajili yake yeye aliyewajulisha, tena kwa ajili ya mioyo isiyojua maana, isilemewe![#1 Kor. 8:7.]
29Sisemi hapa moyo wako unaojua maana, ila wa yule mwingine. Maana visivyo vya mwiko kwangu, vitaumbuliwaje na moyo wa mwingine asiye hivyo?
30Mimi ninapovila kwa kugawiwa, ninabezwaje kwa vile, ninavyovipokea kwa Mungu?[#1 Tim. 4:4.]
31Basi, mkila au mkinywa au mkifanya lo lote jingine, yafanyeni yote, yamtukuze Mungu![#Kol. 3:17.]
32Jiangalieni, msiwakwaze Wayuda wala Wagriki wala wateule wake Mungu![#Rom. 14:13.]
33Kama nami, nawapendeza wote kwa mambo yote, maana siyatafuti yanifaliayo mimi mwenyewe, ila yawafaliayo wale wengi, wapate kuokoka.[#1 Kor. 9:20-22.]