1 Wakorinto 11

1Niigeni mimi, kama nami ninavyomwiga Kristo![#1 Kor. 4:16; Fil. 3:17.]

Jinsi inavyowapasa waume na wake kuomba.

2Nawasifu ninyi, ya kuwa mnanikumbuka po pote, mkashikamana nayo maagizo yangu, kama nilivyowaagiza.

3Lakini nataka, mjue, ya kuwa kichwa cha kila mume ni Kristo, nacho kichwa cha mke ni mume, nacho kichwa cha Kristo ni Mungu.[#1 Kor. 3:23; Ef. 5:23.]

4Kila mume akiomba au akifumbua Neno na kuvaa kichwani, hukipatia kichwa chake soni.[#1 Kor. 12:10; 14:1.]

5Lakini kila mke akiomba au akifumbua Neno pasipo kuvaa kichwani, hukipatia kichwa chake soni, maana hujifananisha kuwa mamoja, kama wenye kunyolewa walivyo.

6Maana mke asipovaa kichwani, naye akatwe nywele! Lakini mke akiona soni ya kukatwa nyuwele au kunyolewa avae kichwani!

7Maana mume haimpasi kuvaa kichwani, kwani yeye ubwana wake hufanana nao wake Mungu; lakini mke ubwana wake ndio uleule wa mume.[#1 Mose 1:27.]

8Maana walipoumbwa, mume hakutoka katika mke, ila mke alitoka katika mume.[#1 Mose 2:22-23.]

9Tena mume hakuumbwa kwa ajili ya mke, ila mke aliumbwa kwa ajili ya mume.[#1 Mose 2:18.]

10Kwa hiyo imempasa mke kushurutishwa kuvaa kichwani kwa ajili ya malaika.

11Kisha wakiwa wa Bwana, hakuna, mke anachokuwa pasipo mume, wala hakuna, mume anachokuwa pasipo mke.

12Kwani kama mke atokavyo katika mume, vivyo hivyo hata mume huzaliwa na mke; lakini yote hutoka kwake Mungu.

13Yapambanueni ninyi kwa ninyi, kama inampasa mke kuomba mbele ya Mungu pasipo kuvaa kichwani!

14Navyo mlivyoumbwa haviwafundishi, ya kuwa mume haimpasi kamwe kuwa na nywele ndefu?

15Lakini mke akiwa na nywele ndefu, ni pambo lake zuri. Maana amepewa nywele ndefu, ziwe mavazi yake.

16Lakini kama yuko anayependa mabisho, basi, mazoea kama hayo hayako wala kwetu wala po pote palipo na wateule wa Mungu.

Chakula cha Bwana.

17Lakini liko neno, sharti niliseme waziwazi, silisifu, ni hili: Hamkutanii mema, ila mabaya.[#1 Kor. 11:22.]

18Kwani kwanza nasikia, ya kuwa hapo, mnapokutania wateule na wateule, yako magawanyiko, nami menginemengine nayasadiki.[#1 Kor. 1:1-12; 3:3.]

19Kwani matengano hayana budi kuwa kwenu, kusudi walio wakweli kwenu waonekane.[#5 Mose 13:3; Mat. 18:7; 1 Yoh. 2:19.]

20Ninyi mnapokutania pamoja, siko kukila Chakula cha Bwana.

21Kwani mnapokula, kila mmoja huanza kunyang'anya chakula chake mwenyewe; kwa hiyo mwingine yuko na njaa, mwingine amelewa.[#Yuda 12.]

22Je, hamna nyumba zenu za kuliamo na kunyweamo? Au mwawabeza wateule wake Mungu mkiwatia soni wasio na kitu? Niwaambieje? Niwasifu? La! Katika hayo siwasifu.[#Yak. 2:5-6.]

23*Maana mimi nalipewa na Bwana, niliyowapa nanyi: Bwana Yesu usiku ule, alipotolewa, akatwaa mkate,[#Mat. 26:26-28; Mar. 14:22-24; Luk. 22:19-20.]

24akashukuru, akaumega, akasema: Twaeni, mle! Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyizeni hivyo, mnikumbuke!

25Vivyo hivyo akakitwaa nacho kinyweo, walipokwisha kula, akisema: Kinyweo hiki ndicho Agano Jipya katika damu yangu. Fanyizeni hivyo, kila mtakapokinywea, mnikumbuke!

26Kwani kila mnapoula mkate huu, mkakinywea nacho kinyweo hiki, kutangazeni kufa kwake Bwana, mpaka atakapokuja![#Mat. 26:29.]

Kujichunguza mwenyewe.

27Kwa hiyo kila anayejilia tu mkate huo na kujinywea tu kinhweo cha Bwana atajionea mapatilizo ya mwili na damu ya Bwana.[#1 Kor. 11:21-22; Ebr. 6:6.]

28Sharti mtu ajichunguze mwenyewe, kisha aule mkate huo, akinywee nacho kinyweo hicho![#Mat. 26:22; 2 Kor. 13:5.]

29Maana mwenye kujilia na kujinywea tu hujilia mapatilizo, hujinywea mapatilizo, kwani haupambanui mwili wa Bwana.

30Kwa hiyo kwenu wako wengi walio wanyonge na wagonjwa, nao waliolala si wachache.[#1 Kor. 15:20.]

31Lakini tunapojichunguza wenyewe hatutapatilizwa.

32Ila tukipatilizwa na Bwana tunaonywa, tusije kuhukumiwa pamoja nao wa ulimwengu huu.*[#Ebr. 12:5-6.]

33Kwa hiyo, ndugu zangu, mnapokutania kula, sharti mngojane!

34Mtu akiwa na njaa ale mwake, kwamba msikutanie mapatilizo! Nayo yaliyosalia nitayaagiza nitakapokuja.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania