The chat will start when you send the first message.
1Lakini kwa ajili ya mchango, watakatifu wanaochangiliwa, fanyeni nanyi, kama nilivyowaagiza wateule wa Galatia![#Tume. 11:20; 2 Kor. 8:9; Gal. 2:10.]
2Kila siku ya kwanza ya juma kila mmoja wenu na aweke kwake na kuyalimbika yapatanayo na mapato yake, kisha ayachanganye yote, maana machango yasianzwe hapo, nitakapofika![#Tume. 20:7.]
3Lakini ndipo nifike, wale, mtakaowachagua ninyi, nitawatuma na barua, wavipeleke vipaji vyenu Yerusalemu.
4Lakini vikiwa vingi vya kupasa, niende nami, watakwenda pamoja nami.
5Lakini nitafika kwenu, nitakapokwisha kupita huko Makedonia. Kwani Makedonia nitapita tu;[#Tume. 19:21.]
6lakini kwenu, kama vinapatikana, nitakaa, labda nitamaliza kwenu siku za kipupwe, ninyi mpate kunisindikiza huko nitakakokwenda[#Rom. 15:24.]
7Kwani sasa sitaki kuonana nanyi kwa kupita tu; kwani nangojea, nikae kwenu kitambo cha siku, Bwana akipenda.[#Tume. 18:21; 20:2.]
8Lakini huku Efeso nitakaa mpaka sikukuu ya Pentekote.[#Tume. 19:1,8-10.]
9Kwani nimefunguliwa mlango mkubwa, tena kazi inaendelea, ijapo wabishi wawe wengi.[#2 Kor. 2:12; Kol. 4:3; Ufu. 3:8.]
10Lakini Timoteo atakapofika, mmtazame, akae kwenu pasipo woga! Kwani naye anaifanya kazi ya Bwana kama mimi.[#1 Kor. 4:17; Fil. 2:20.]
11Pasiwe anayembeza! Ila msindikizeni na kupatana, afike kwangu! Kwani tunamngojea mimi na ndugu.[#1 Kor. 16:6; 1 Tim. 4:12.]
12Lakini kwa ajili ya ndugu yetu Apolo mjue, ya kuwa nimemhimiza mara kwa mara, aje kwenu pamoja na hao ndugu; lakini hakutaka kabisa kwenda sasa. Lakini atakuja, patakapomfalia.[#1 Kor. 1:12.]
13Kesheni! Kukalieni kumtegemea Bwana, mwe waume wenye nguvu![#Ef. 6:10.]
14Mambo yenu yote yafanywe katika upendano!
15Ndugu, nitakalo tena, ni hili: mwawajua akina Stefana, ya kuwa ndio malimbuko ya nchi ya Akea, tena wamejitoa wenyewe, waje wawatumikie watakatifu.[#1 Kor. 1:16; Rom. 16:3.]
16Kwa hiyo nanyi mwatii walio hivyo na kila aliye mwenzao wa kazi na wa masumbuko![#Fil. 2:29.]
17Nimefurahiwa na kuja kwake Stefana na Fortunato na Akaiko, kwani ndio walionifanyizia, ambavyo ninyi hamkuweza kunifanyizia.
18Kwani wameituliza roho yangu nazo roho zenu. Basi, watambueni walio hivyo![#1 Tes. 5:12.]
19Wateule wote walioko Asia wanawasalimu. Akila na Puriskila pamoja nao wote wanaokusanyika nyumbani mwao wanawasalimu sana, kwa kuwa m wa Bwana.[#Tume. 18:2,18,26; Rom. 16:3-5.]
20Nao ndugu wote wanawasalimu. Mwamkiane mkinoneana, kama watakatifu walivyozoea![#Rom. 16:16; 2 Kor. 13:12; 1 Petr. 5:14.]
21Hii salamu yangu mimi Paulo naiandika kwa mkono wangu.[#Kol. 4:18; 2 Tes. 3:17.]
22Mtu asiyempenda Bwana na awe ameapizwa! Bwana anakuja.[#Gal. 1:8-9.]
23Upole wa Bwana Yesu uwakalie ninyi![#Ufu. 22:20.]
24Upendo wangu wa kuwapenda ninyi, kwa kuwa m wake Yesu Kristo, uwakalie ninyi nyote! Amin.