The chat will start when you send the first message.
1*Hivyo kila mtu atuwazie sisi kuwa watumikizi wa Kristo na watunzaji wa mafumbo yake Mungu.[#Tit. 1:7.]
2Tena kwa watunzaji halitafutwi jingine, ni hili tu, ajulike kuwa mwelekevu.[#Luk. 12:42.]
3Kwangu mimi si kitu, nikihukumiwa nanyi au na wengine wanaohukumu kimtu; nami mwenyewe sijihukumu,
4kwani sinacho kibaya, ninachokijua moyoni. Lakini kwa hivyo si mwongofu; ila atakayenihukumu ni Bwana.[#Sh. 143:2.]
5Kwa hiyo msihukumu neno lo lote siku hizi, mpaka Bwana atakapokuja; yeye ndiye atakayeyatia mwangani yaliyofichwa gizani; tena ndiye atakayeyafumbua waziwazi mawazo ya mioyo. Hapo ndipo, kila mtu atakapoonea sifa yake kwa Mungu.*[#1 Kor. 3:8; Mbiu. 12:14.]
6Ndugu, kwa ajili yenu nimeyasema haya kama mfano wa mimi na Apolo, mpate kujifundishia kwetu sisi, msijikweze kupapita hapo palipoandikwa kwamba: Mtu asijitutumue kuwa mkuu kuliko mwenziwe na kumpunguza mwingine![#Rom. 12:3; 1 Tim. 1:6-7.]
7Je? Yuko anayekupatia wewe macheo zaidi? Unacho kitu gani, usichopewa? Lakini kama umepewa, wajivuniaje, kama hukupewa?
8Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata mali nyingi, mkatwaa nao ufalme, msiopewa na sisi. Tunataka sana, mwe wafalme, nasi tupate kuwa wafalme wenzenu.
9Maana naona, ya kuwa Mungu ametuweka sisi mitume kuwa wa mwisho, kama watu wanaopaswa na kuuawa, kwani sisi ndio wanaotazamwa nao wa ulimwengu wote: malaika, hata watu.
10Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi m wenye akili kwa kuwa naye Kristo. Sisi tu wanyonge, ninyi m wanguvu. Ninyi mwatukuzwa, lakini sisi twabezwa.
11Mpaka saa hii ya sasa maumivu yetu yako, ni haya: njaa na kiu na uchi na mapigo na kukosa kikao;
12twasumbuka tukifanya kazi na mikono yetu sisi. Tukitukanwa twaombea mema; tukifukuzwa twavumilia;[#1 Kor. 9:15; Sh. 109:28; Luk. 6:27-28; Tume. 18:3; 20:34; Rom. 12:14; 1 Tes. 2:9; 2 Tes. 3:8.]
13tukisingiziwa twabembeleza. Tumekuwa kama taka za ulimwengu, kama kifusi chao wote hata sasa hivi.
14Siyaandiki haya, niwatie soni, ila nawaonya kama watoto wangu, ninaowapenda.
15Kwani ingawa mnao wafunzi maelfu katika Kristo, lakini hamnao baba wengi. Kwani mimi ndiye niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa kuwapigia hiyo mbiu njema.[#Gal. 4:19.]
16Kwa hiyo nawaonya, mniige mimi.[#1 Kor. 11:1.]
17Kwa sababu hii nimemtuma Timoteo kwenu, huyu ni mtoto wangu mpendwa na mwelekevu katika Bwana. Yeye atawakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama ninavyowafundisha wateule wote po pote.[#Tume. 19:22.]
18Lakini wako wanaojivuna, kwamba mimi siji kwenu.
19Lakini nitakuja kwenu upesi, Bwana akitaka; ndipo, nitakapozitambua nguvu zao, wanazojivunia, si maneno yao tu.[#Tume. 18:21; Yak. 4:15.]
20Maana ufalme wa Mungu sio wa kujisemea, ila uko na nguvu.[#1 Kor. 2:4; Luk. 17:20.]
21Mnataka nini? Nije kwenu nikishika fimbo, au nije mwenye upendo na roho ya upole?