The chat will start when you send the first message.
1Inakuwaje, mtu wa kwenu aliye na jambo na mwenziwe akijipa moyo wa kuja kushtaki mbele yao walio wapotovu, asije mbele yao walio watakatifu?
2Au hamjui, ya kuwa watakatifu watauhukumu ulimwengu? Ikiwa ulimwengu utahukumiwa nanyi, isiwapase kuamulia mambo yaliyo madogo?[#Dan. 7:22; Mat. 19:28; Ufu. 3:21.]
3Hamjui, ya kuwa tutahukumu malaika? Nayo ya huku nchini yasitupase?
4Mkitaka kushtakiana mambo ya huku nchini, inakuwaje, mkiwaketisha katika kiti cha uamuzi wale wanaobezwa kwa wateule?
5Haya nayasemea kuwatia soni. Je? Kwenu hakuna hata mmoja mwenye werevu wa kweli awezaye kuamua ndugu na mwenzake?
6Kwenu sharti ndugu na ndugu washtakiane, kisha wapelekane kwao wasiomtegemea Mungu?
7Kweli hayo mambo yote ya kushtakiana ninyi kwa ninyi ni kukosa utimilifu. Sababu gani hamtaki kupotolewa? Tena sababu gani hamtaki kunyang'anywa?[#Mat. 5:38-41; 1 Tes. 5:15; Ebr. 10:34; 1 Petr. 3:9.]
8Lakini ninyi mwapotoana, mwanyang'anyana wenyewe, tena m ndugu!
9Au hamjui, ya kuwa wapotovu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msipotelewe! Wagoni na watambikia vinyago na wavunja unyumba na walegevu na wenye kulalana
10na wezi na wenye choyo na walevi na wenye matusi na wanyang'anyi, hao wote hawatautwaa ufalme wa Mungu.[#Gal. 5:19-21.]
11Hata kwenu wako walio hivyo. Lakini mmeoshwa, tena mmetakaswa, mkaupata wongofu uliomo katika Jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho ya Mungu wetu.[#Tit. 3:3-7.]
12Kwangu mimi hakuna cho chote chenye mwiko, lakini sivyo vyote vifaavyo: kwangu mimi hakuna cho chote chenye mwiko, lakini kitakachonishinda sikitaki kamwe.[#1 Kor. 10:23.]
13Vyakula ni vya tumbo, nalo tumbo ni la vyakula; naye Mungu atavitowesha vyote viwili. Lakini mwili sio wa ugoni, ila wa Bwana, yeye Bwana ni mwenye mwili.[#1 Tes. 4:3-5.]
14Mungu alimfufua Bwana, vivyo hivyo atatufufua hata sisi kwa nguvu yake.[#1 Kor. 15:15,20; Rom. 8:11; 2 Kor. 4:14.]
15Hamjui, ya kuwa miili yenu ni viungo vyake Kristo? Je? Nivichukue viungo vyake Kristo, nivigeuze kuwa vya ugoni? La, sivyo![#1 Kor. 12:27.]
16Au hamjui, ya kuwa mwenye kugandamiana na mke mgoni amekwisha kuwa mwili mmoja naye? Maana asema: Hao wawili watakuwa mwili mmoja.[#1 Mose 2:24.]
17Lakini mwenye kugandamiana na Bwana watakuwa roho moja.[#Yoh. 17:21-22; Gal. 2:20; Ef. 5:30.]
18Ukimbieni ugoni! Kosa lo lote, mtu atakalolifanya, liko nje ya mwili wake, lakini mgoni huukosea mwili wake mwenyewe.
19Au hamjui, ya kuwa miili yenu ni nyumba yake Roho Mtakatifu awakaliaye? Ndiye, mliyepewa na Mungu, ninyi ham wenye ninyi.[#1 Kor. 3:16.]
20Mmenunuliwa pakubwa, kwa hiyo mtukuzeni Mungu miilini na rohoni mwenu! Maana ni yake Mungu.[#1 Kor. 7:23; Fil. 1:20; 1 Petr. 1:18-19.]