The chat will start when you send the first message.
1Wapendwa, msiitikie kila roho, ila zijaribuni roho, kama zimetoka kwa Mungu! Kwani wafumbuaji wa uwongo wengi wametokea ulimwenguni.[#Mat. 7:15; 1 Tes. 5:21.]
2Hapo ndipo, mtakapoitambua roho ya Mungu: kila roho inayoungama, ya kuwa Yesu Kristo amekuja mwenye mwili wa kimtu, imetoka kwa Mungu.
3Lakini kila roho isiyomwungama Yesu haikutoka kwa Mungu. Hiyo ndiyo roho ya Mpinga Kristo, mliyoisikia, ya kuwa inakuja; tena sasa imekwisha kuwamo humu ulimwenguni.[#1 Yoh. 2:18; 1 Kor. 12:3.]
4Vitoto, ninyi m wa Kimungu, tena mmewashinda wale, kwani yeye alimo mwenu ni mkubwa kuliko yeye aliomo humu ulimwenguni.
5Wale ni wa kiulimwengu; kwa hiyo husema ya kiulimwengu, nao wa kiulimwengu huwasikia.[#Yoh. 15:19.]
6Sisi tu wa Kimungu; naye amtambuaye Mungu hutusikia sisi, lakini asiye wa Kimungu hatusikii sisi. Hapo twaitambua roho, kama ni ya kweli au ya upotevu.[#Yoh. 8:47.]
7Wapendwa, tupendane sisi kwa sisi! Kwani upendo ni wa Kimungu. Kila mwenye kupenda amezaliwa naye Mungu, naye humtambua Mungu.
8Asiyependa hakumtambua Mungu kwamba: Mungu ni upendo.[#1 Yoh. 4:16.]
9*Upendo wake Mungu wa kutupenda sisi umeonekana waziwazi hapo, Mungu alipomtuma Mwana wake wa pekee kuja ulimwenguni, sisi tupewe naye uzima.[#Yoh. 3:16.]
10Humu ndimo upendo: sio sisi tuliompenda Mungu, ila yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwana wake kuwa kole kwa ajili ya makosa yetu.[#1 Yoh. 2:2.]
11Wapendwa, kama Mungu alitupenda hivyo, imetupasa nasi kupendana.[#Mat. 18:33.]
12Hakuna mtu aliyemwona Mungu hata kale; tukipendana, Mungu hukaa mwetu, upendo wake ukatimilika mwetu.[#Yoh. 1:18.]
13Hapa ndipo, tunapotambua, kama tumo mwake yeye, kama yeye naye yumo mwetu, tukiwa na Roho wake, ambaye alitugawia.[#1 Yoh. 3:24.]
14Nasi tumeviona, tukavishuhudia, ya kuwa Baba amemtuma Mwana, awe mwokozi wa ulimwengu.*[#Yoh. 3:17.]
15Ye yote atakayeungama kwamba: Yesu ni mwana wake Mungu, basi, Mungu hukaa mwake huyo, naye mwake Mungu.[#1 Yoh. 5:5.]
16Nasi tumeutambua, tukautegemea upendo wake Mungu wa kutupenda sisi.[#1 Yoh. 4:8.]
*Mungu ni upendo; naye mwenye upendo hukaa mwake Mungu, naye Mungu hukaa mwake yeye.
17Upendo, tupendwao nao, unatimilika hapo, tukiweza kuishangilia siku ya hukumu; kwani yeye alivyo, ndivyo, tulivyo na sisi humu ulimwenguni.[#1 Yoh. 2:28.]
18Woga haumo katika upendo, ila upendo uliotimilika huufukuza woga, kwa sababu woga huhangaisha. Naye aliye mwenye woga bado hajautimiliza upendo.
19Sisi na tumpende! Kwani yeye alianza kutupenda sisi.
20Mtu akisema: Nampenda Mungu, akamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Kwani asipompenda ndugu yake, anayemwona, hawezi kumpenda Mungu, asiyemwona,
21maana agizo hili tumepewa naye kwamba: Mwenye kumpenda Mungu sharti ampende na ndugu yake!*[#Mat. 22:37-40; Mar. 12:29-31.]